Unaweza kuona ni kama miujiza, timu iliyokuwa Ligi Kuu Bara msimu uliopita, taarifa zinakufikia msimu ujao itacheza daraja la pili.
Toto African, msimu ujao itakuwa daraja la pili baada ya msimu uliopita kuteremka ikitokea ligi kuu na msimu huu imecheza Ligi Daraja la Kwanza.
Timu hiyo kutoka Mwanza, imekutana na kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Dodoma FC na kudhibitisha safari yake ya kwenda daraja la pili.
Kipigo hicho kinaifanya Toto African kuendelea kubaki na pointi 10 mkiani mwa kundi C lenye timu nane huku Biashara Mara na Alliance zikipanda hadi Ligi Kuu Bara na Dodoma FC, Rhino Rangers, JKT Oljoro, Transit Camp na Pamba zikisubiri msimu ujao wa daraja la kwanza.
No comments:
Post a Comment