BAADA YA OKWI UPIGWA NGUMI UWANJANI JANA MANARA AJA NA KAULI HII>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Monday, February 5, 2018

BAADA YA OKWI UPIGWA NGUMI UWANJANI JANA MANARA AJA NA KAULI HII>>

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha Klabu ya Simba Haji Sunday Manara amesema hali ya Emmanuel Okwi baada ya kupigwa kooni na beki wa Ruvu Shooting Mau Bofu katika dakika ya 45.
Akitoa taarifa hiyo Manara amesema Okwi anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa huduma ya kwanza na kwamba atajiunga na wenzake katika mazoezi leo kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam FC.
“Okwi anaendelea vizuri, unajua baada ya kupigwa ngumi kwenye koo kupumua ilikuwa tabu, lakini kwa sasa anaendelea vizuri japo maumivu kidogo yapo, Timu inaingia kambini Jumatatu mpaka kwenye mechi ya Azam na yeye atakuwepo kambini,” Manara amesema.
Kuhusu majeruhi wengine Manara amesema Juuko Murushid alikuwa na homa ya tumbo ‘Typhoid’ na anaendelea kupata nafuu lakini pia James Kotei ambaye hakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.
“Kotei alikuwa na maumivu kidogo lakini Wote hao watajiunga na wenzao kwenye kambi siku ya Jumatatu kujiandaa na mchezo dhidi ya Azam,” amesema.
Manara ameendelea kuwaomba mashabiki wa Simba kuendelea kuiunga mkono timu yao kwa kuishangilia kwani wanaamini hatua za kuelekea kwenye ubingwa zimebaki chache.
Katika mchezo huo wa Jumapili uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba waliibuka na ushindi wa mabao 3-0 mabao ambayo yamefungwa na John Raphael Bocco pamoja na Mzamiru Yassin.

No comments:

Post a Comment