Uamuzi wa beki Mwinyi Haji kutaka kuachana na Yanga hautabadilika.
Rafiki yake wa karibu ameiambia SALEHJEMBE, Mwinyi amesisitiza suala hilo na lazima ataondoka.
"Unajua Mwinyi amewaambia hadi wazazi wake na wenyewe wamekubaliana naye. Anaona ni wakati wa kutimiza ndoto yake ya kucheza nje ya Tanzania.
"Amekuwa akisisitiza, lakini inaonekana kama viongozi wa Yanga wanamchelewesha ili dirisha la Kenya lifungwe," alisema rafiki yake huyo ambaye hakutaka kutajwa.
Mwinyi amekuwa akisisitiza anataka kuondoka Yanga baada ya kupata ofa ya kuichezea timu kongwe ya Kenya ya AFC Leopards ambayo imemuona katika michuano ya Kombe la Chalenji akiitumikia Zanzibar Heroes iliyofika fainali.

No comments:
Post a Comment