MAKALA FUPI : HII NDIO YANGA IYOANZISHWA MIAKA YA 1935 IJUE ZAIDI KLUB HII GHALI DUNIANI>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Wednesday, January 3, 2018

MAKALA FUPI : HII NDIO YANGA IYOANZISHWA MIAKA YA 1935 IJUE ZAIDI KLUB HII GHALI DUNIANI>>

KWELI MBABE AKILI, WANYONGE LAZIMA WAFURAHI
CHEKI HII HISTORIA

*HISTORIA FUPI YA YANGA*

Yanga  ilianzishwa mnamo mwaka 1935 na inasemekana ndo klabu kongwe na yenye mafanikio zaidi hapa nchini. Klabu hii ilianzishwa na wazalendo halisi wa nchi hii waliokuwa wakiji shughulisha na uchuuzi wa nazi na samaki na muda wao wa jioni ulipofika
walikuwa wakijumuika pamoja kusakata kabumbu na hapo ndipo ilizaliwa Yanga.

Kama  hiyo haitoshi wazalendo hawa waliendelea kujikusanya kwa pamoja na kuanza mishemishe za kusaka uhuru wa nchi hii, na ndipo tarehe 9 December  mwaka 1961 Tanganyika ikapata uhuru,
hivyo kama tutazungumzia uhuru wa taifa hili basi hatusiti kwa namna moja au nyingine kuitaja Yanga, na kwa heshima yake inatakiwa unapoitaja Yanga  kama umekaa basi unatakiwa usimame

*MAFANIKIO.*
Yanga  ndio timu iliyochukua ubingwa wa ligi ya bara mara nyingi zaidi, na ndio klabu inayofahamika zaidi kitaifa na kimataifa kwa sababu ndiyo klabu iliyopeperusha vizuri Bendera  ya taifa hili la
Tanzania  nje ya mipaka.

Na  kama hiyo haitoshi Yanga  ndiyo klabu yenye washabiki wengi zaidi ndani na nje ya nchi, ndani ya Africa  na dunia kwa ujumla. Na pia Yanga  ndiyo klabu ya mwanzo hapa nchini au hata Africa
mashariki kwa ujumla kwa kuwa na makao makuu sambamba na uwanja wa mazoezi ambao unajulikana kwa jina la Kaunda, jina la
muasisi na mpigania uhuru mwengine wa taifa la Zambia
Mheshimiwa Kenneth  Kaunda.

Mfumo huu wa kuwa na makao makuu pamoja na uwanja wa
mazoezi ni wa timu kubwa barani ulaya na dunia kwa ujumla. Yanga  pia ndio timu ya kwanza kuwa na gazeti hapa nchini. Gazeti
hili linajulikana kama *"Yanga imara"*. Lilipotoka katika wiki ya kwanza liliuzwa takribani nakala 500,000 nchi nzima na baadhi ya nchi za jirani.

Mfumo wa kuwa na gazeti la klabu pia umeigwa na baadhi ya klabu hapa nchini lakini unaonekana kusua sua katika mauzo na hata ukisoma nakala ya gazeti lao utakuta limejaa matangazo ya waganga tu.

Yanga  ndo timu pekee iliyowahi kuuza mchezaji nje ya nchi na kung'aa katika vilabu mbali mbali barani ulaya, mchezaji huyu
alijulikana kama *Nonda Shaaban* al maarufu kama *"papii"*. Nonda ambaye aliwahi kutamba na mashujaa hawa wa jangwani amepata kuchezea vilabu kama Val Profesional ya South  Africa ,
FC Zurich  ya uswis, Stade rennes na AS Monaco  zote za
ufaransa, AS Roma  ya Italia  akicheza pamoja na Francesco  Totti, Blackburn  ya uingereza na baadae akakipiga katika klabu ya Galatasaray yenye maskani yake katika uwanja wa Ali Sami  Yen nchini Uturuki.

Na  hapa ndipo tunapoitofautisha Yanga  na vilabu vingine vya soka hapa nchini ambavyo wachezaji wake huuzwa Burundi, Rwanda  na Kenya ambako hakuna soka la ushindani. Pia Yanga ndo timu ya kwanza hapa nchini kuongozwa na Rais. Pia Yanga  ndo timu ya kwanza kuwa na mfumo wa wanachama kuwa wana hisa wa klabu kama timu nyingi za ulaya, hivyo kumfanya kila mwanachama kuhusika kikamilifu katika mipango, na malengo ya klabu, tofauti na majirani zetu ambao hapo mwanzo mfumo wao wa uongozi ulikuwa haueleweki na hata mishahara ya wachezaji wanalipwa
kimkanda mkanda na inafika kipindi mchezaji anakaa miezi minne hajalipwa mshahara mwisho wanatimkia kucheza ligi za mchangani.

*MAFANIKIO NJE YA MIPAKA.*
Yanga kama Yanga  ndo timu pekee iliyowahi kuchukua kombe linalotambuliwa na Shirikisho la soka barani Africa CAF na Shirikisho la soka duniani FIFA.

 Itakumbukwa tu Yanga
waliwafunga Express ya Uganda  kwa goli 3-1 katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la klabu bingwa afrika mashariki na kati na mechi ya fainali walitakiwa wakipige na SC Villa. Yanga waliwacharaza bila huruma SC Villa goli 2-1 katika uwanja wa Nakivubo kwenye mechi ya fainali ya kombe lililokuwa na msisimko kipindi hicho la klabu bingwa Africa  Mashariki  na kati na
kupelekea serikali ya Tanzania  kutuma ndege mpaka katika
uwanja wa ndege wa Entebe kwenda kuwachukua Waheshimiwa waliolitoa taifa kimasomaso yaani Yanga. Hivyo kuweka adabu kwa waganda ambao hawawezi kuisahau Yanga  maishani mwao.

Yanga  katika mechi hiyo iliwakilishwa na:
1) Steven  Nemes
2) Mwanamtwa kihwelu
3) Kenneth  Mkapa
4) Willy  Mtendamema
5) Issa Athuman
6) Method Mogella
7) Steven  Mussa
8) Hamis  Thobias Gagarino
9) Said  Mwamba  Kizota
10) Mohamed  Hussein  Chinga one
11) Edibily  Jonas  Lunyamila

Pia  Yanga walikuwa na bunduki nje kwenye benchi kama Willy Martin, Rifat Said, Aboubakar Salum "sure boy" David  Mwakalebela "MP" na wengine wengi ambao walikuwa ni miiba kwa waganda.

Katika mechi hiyo mnamo dakika ya 81 beki mahiri wa Villa na timu ya taifa ya Uganda  marehemu Paul Hasule alivua jezi na kutoka
nje kwa kile ambacho mwenyewe alikiri kuwa ameshindwa kumkaba
winga wa Yanga  Edibily  lu6nyamila, lakini alilazimishwa na kocha
wake kumaliza mechi kutokana na aibu iliyokuwa inawakabili.
 Kutokea hapo waganda walitekwa akili kutokana na kabumbu safi lililoonyeshwa na Yanga  na kupelekea daladala nyingi nchini humo kuandikwa majina kama *"Lunyamila  trans"* *kizota trans* au hata
wengine walifuta majina ya saloon  zao na kuandika *"Gagarino hair salon"* na mpaka leo hii waganda wakisikia timu kutoka Tanzania inakwenda huko wanauliza *"Je ni Yanga ?"*.
Na  baada ya ushindi huo mwanamuziki nguli wa Afrika marehemu *Kabasele Yampanya* al maarufu kama *Peppe Kalle* alitunga wimbo
wa kuisifia timu hiyo baada ya kuonyesha dhahili kiwango cha juu na kuvutia washabiki wengi wa soka kitu ambacho hakijawahi kufanywa na klabu yoyote nyingine hapa nchini.

*HISTORIA ISIYO SAHAULIKA*
Mwaka 1972 katika pambano la watani wa jadi lililokuwa lifanyike katika uwanja wa Taifa, Watanzania walishuhudia kituko cha mwaka pale klabu  ya Simba  ya Dar es salaam ilipoishia
Chang'ombe na kugeuza basi na kurudi katika mtaa wa Msimbazi na kufanya timu ya Yanga  ya Tanzania  kupewa ushindi baada ya mpinzani kufyata mkia na kutokomea vichakani.

Mnamo pia tarehe 13 mwezi novemba mwaka 1991 katika uwanja huo huo wa Taifa  timu ya Yanga  ya Tanzania waliingia uwanjani na
basi la Sharuksi lililokuwa likimilikiwa na mfadhili wa yanga wa kipindi hicho marehemu Abbas  Gulamali, Timu  ya soka ya Simba ya  iliweka mpira kwapani wakati wa mapumziko na kutokomea kusiko julikana. Na kauli hii ya kuweka mpira kwapani ilitolewa na mtangazaji
aliyekuwa anatangaza soka redio Tanzania  siku hiyo ndugu *Charles Hillary* na magazeti kama Motomoto, Mfanyakazi, Uhuru  na
Mzalendo ya kipindi hicho yalipambwa na kichwa kikubwa cha habari *"Mgonjwa Atema Dawa"* Na kuuweka mpira huko kwapani kulifuatia vipigo mfululizo vya August 31, October  9 lakini hii ilitanguliwa na kipigo cha Said Sued "Scud" cha mei 18.

Baadhi ya mashujaa waliowahi kukipiga Yanga  miongoni mwao ni Rifat Said, Joseph Katuba, Peter Manyika, Anwar Awadh, Salum kabunda "ninja", Godwin  Aswile "baba subi" au scania, Said  Zimbwe, Thomas Kipese, Joseph Lazaro, Omar  Hussein, Constantine  Kimanda, Sanifu lazaro "tingisha" na wengine wengi.

Hili nililokupa hapo ni tone tu la maji, ila bahari ntakupa siku nyingine. Na hii ndo Yanga, klabu bora kabisa hapa nchini

No comments:

Post a Comment