Wakati Simba wakiwa nyumbani kwa Balozi wa Uturuki nchini Tanzania ambako walipata mwaliko, yeye alikabidhiwa ile tuzo yake ya mchezaji bora wa Desemba wa Simba.
Lakini kama hiyo haitoshi, Manula alikabidhiwa fulana maalum ya klabu maarufu nchini Uturuki ya Galatasaray, jamabo ambalo wengi wamelichukulia kama baraka.
Inaonekana amepewa baraka na hali ya kujiamini kuendelea kujituma zaidi ikiwezekana siku moja kutimiza ndoto ya kucheza nje ya Tanzania hata kama si Uturuki.
Manula amekuwa akiendelea kukidumisha kiwango chake kwa muda hata kabla ya kutua Simba wakati akiitumikia Azam FC.
Kwa sasa ndiye kipa namba moja wa Tanzania na anaonekana ndiye bora zaidi kwa kipindi hiki.
No comments:
Post a Comment