Ikiwa jana ilikuwa December 31, 2017 ilikiwa siku ya mwisho, weekend ya mwisho na mwisho wa mwezi wa mwisho ndani ya mwaka huu, kuna rekodi kibao zimewekwa kwenye mchezo wa VPL kati ya Mbao dhidi ya Yanga uliochezwa uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
Mbao wameikalisha Yanga katika mchezo huo kwa bao 2-0 huku magoli yote yakifungwa na kijana Habib Haji Kiyombo.
Yanga wamepoteza mechi ya tatu dhidi ya Mbao kwenye uwanja wa CCM Kirumba. Mara ya kwanza walipoteza mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (1-0) wakapoteza mchezo wa mwisho wa ligi msimu uliopita (Mbao 1-0 Yanga) na leo December 31, 2017 (Mbao 2-0 Yanga)
Yanga wamepoteza mechi ya kwanza msimu huu baada ya kucheza michezo11 bila kupoteza. Katika mechi 11 walizocheza kabla ya mchezo wa leo, Yanga walikuwa wameshinda mechi 5 na kutoka sare katika michezo 6.
Mbao wameshinda mechi yao ya tatu baada ya kucheza mechi 12 kwenye ligi msimu huu, ni mechi ya pili kushinda kwenye uwanja wa CCM Kirumba msimu huu. Walikuwa wameshinda michezo miwili tu kati ya 11 kabla ya mchezo wa leo (Kagera Sugar 0-1 Mbao, Mbao 1-0 Mwadui na leo Mbao 2-0 Yanga).
Kwa mara ya kwanza Mbao wameshinda kwa magoli zaidi ya moja katika mechi tatu walizofanikiwa kushinda msimu huu, mechi mbili walizoshinda msimu huu walishinda kwa goli 1-0. (Kagera Sugar 0-1 Mbao, Mbao 1-0 Mwadui na Mbao 2-0 Yanga).
Mbao haijapoteza mechi hata moja dhidi ya timu tatu za juu katika raundi ya kwanza msimu huu kwenye uwanja wa CCM Kirumba (Mbao 2-2 Simba, Mbao 0-0 Azam, Mbao 2-0 Yanga).
Habib Kiyombo (aliyefunga magoli mawili vs Yanga) amefikisha magoli saba (7) na kukaa nyuma ya Emanuel Okwi ambaye anaongoza orodha ya wafungaji wa VPL akiwa na magoli nane (8).
Abdallah Shaibu ‘Ninja’ ameanza kwa mara ya kwanza katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara tangu alipojiunga na timu hiyo.
Amisi Tambwe amerejea kwa mara ya kwanza kucheza mechi ya ligi baada ya kupona majeraha. Hakucheza mechi zote 11 za kwanza ambazo Yanga wamecheza.
No comments:
Post a Comment