Nahodha wa Simba, John Raphael Bocco, amesema suala la ufungaji bora kwake litafuatia baada ya kuhakikisha timu inafanya vizuri.
Bocco ambaye aliifungia Simba mabao mawili na kuisadia kuilaza Ndanda FC kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Nangwanda amesema anapambana kuhakikisha Simba inashinda.
"Kwanza ni timu, nataka timu ishinde na tupate pointi tatu. Hili ndiyo suala muhimu zaidi kwangu. Halafu baada ya hapo, litafuatia la ufungaji," alisema.
"Nawashukuru wachezaji wenzangu, tumecheza kwa nguvu na kupambana kwa ajili ya timu na matokeo yamekuwa mazuri."
No comments:
Post a Comment