SIMBA WALAANI KITENDO CHA ERASTO NYONI KUTUPWA NJE STARS, BIFU LAANZIA HAPA>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Friday, November 3, 2017

SIMBA WALAANI KITENDO CHA ERASTO NYONI KUTUPWA NJE STARS, BIFU LAANZIA HAPA>>



*MKUDE, MDATHIR WAITWA STARS, MZAMIRU,ERASTO NYONI WAONDOLEWA*

*nilichanganya jaman kikos kioichotangazwa ni hiki hicho kingine ni under 23 msiwie radhi*

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Salum Mayanga amefanya mabadiliko ya lazima kwa  kuwaita kikosini viungo wa klabu ya Simba Jonas Mkude na Mudathir  Yahya kutoka Azam Fc akiwa anacheza Singida United kwa mkopo, akiwaondoa kikosini Erasto Nyoni na Muzamiru Yassin  baada ya ufafanuzi kutoka FIFA kuhusu kadi nyekundu walizopata katika mchezo uliopita.

Nyoni na Mzamiru walipata kadi nyekundu katika mchezo wa kirafiki kati ya Tanzania na Malawi ambalo ulipigwa hapa hapa nchini na timu hizo kutoka sare ya goli 1-1, gali la Tanzania likifungwa na Simon Msuva huku la Malawi likifungwa na Robert Ng'ambi.

Jonas Mkude na Mudathir  Yahya wanaungana na wachezaji wengine 22 ambao waliitwa na kocha huyo kuingia kambini kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin utakaopigwa November 12 mwezi huu mjini Benin.

Mdathir Yahya anaunga na wachezaji wengine 24 waliotwa na Mayanga October 24 kwa ajili ya mchezo ambao Stars watasafir hadi Benin November 10 na kucheza mchezo huo November 12 huko huko Benin.

Kikosi kilichotangazwa na kocha mkuu wa Taifa Stars Salum Mayanga kinaundwa na  Makipa ni Aishi Manula(Simba), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Singida United).

Mabeki  ni Gadiel Michael (Yanga), Boniface Maganga (Mbao FC), Nurdin Chona(Tanzania Prisons), Abdi Banda (Baroka FC, Afrika Kusini), Kelvin Yondani (Yanga) na Dickson Job (Mtibwa Sugar).

Viungo ni Himid Mao (Azam), Hamis Abdallah (Sonny Sugar, Kenya), Jonas Mkude (Simba), Raphael Daud (Yanga),Simon Msuva (Difaa El Jadidi, Morocco), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (Tenerife, Hispania), Abdul Hilal (Tusker, Kenya), Mohammed Issa (Mtibwa Sugar) na Ibrahim Ajib (Yanga) Mdathir Yahya (Azam Fc), Singida United kwa mkopo.

Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Mbaraka Yusuph (Azam), Elias Maguri (Dhofar, Oman) na Yohana Mkomola (Etoile du Sahel,

No comments:

Post a Comment