CHELSEA HALI SI SHWALI, MMILIKI WA KLABU ROMAN ABROMOVICH KUMFUNGASHIA VILAGO KOCHA MKUU ANTONIO CONTE ENDAPO HATAFANYA VIZURI LEO DHIDI YA MAN U. SOMA CHANZO - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Sunday, November 5, 2017

CHELSEA HALI SI SHWALI, MMILIKI WA KLABU ROMAN ABROMOVICH KUMFUNGASHIA VILAGO KOCHA MKUU ANTONIO CONTE ENDAPO HATAFANYA VIZURI LEO DHIDI YA MAN U. SOMA CHANZO




Mmiliki wa timu ya Chelsea na kocha mkuu hawaongei
Kasulu wadau

Taarifa zinaeleza hali si shwari katika klabu ya Chelsea na sasa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abromovich hana maelewano mazuri na kocha Antonio Conte na siku za usoni hawajawahi kuonana.

Mmiliki wa Chelsea Roman Abromovich huwa ana mahusiano ya karibu sana na makocha wa timu yake na hupenda kuwaweka karibu yake na ndivyo alivyofanya wakati Antonio Conte akijiunga na Chelsea.

Gazeti maarufu la masuala ya michezo la Marca limechapisha habari inayosema kwamba watu hao wawili hawaongei moja kwa moja kwa sasa na kama Conte akitaka kuongea na Abromovich ni lazima amtumie Secretary wake.

Mahusiano kati ya wawili hao yalianza kuwa katika hali mbaya wakati wa dirisha la usajili huku sababu kubwa ikidaiwa ni Conte kutoridhishwa na namna ambavyo klabu ya Chelsea inaendesha dirisha la usajili.

Mbaya zaidi Marca wamesema tayari kuna kikundi cha wachezaji ndani ya Chelsea ambao hawamuungi mkono Antonip Conte na wengi wakichukizwa na kitendo alichomfanyia Diego Costa baada ya msimu kuisha.

Kwa mambo yanayoendelea Chelsea inaonesha wazi huenda huu ukawa msimu wa mwisho kwa Conte kuitumikia Chelsea na kipigo cha bao 3 kwa 0 toka kwa As Roma kimezidi kuchafua hali ya hewa kwa meneja huyo.

Chelsea wana kibarua kigumu zidi ya Manchester United mchezo ambao utamlazimu Conte kushinda laa sivyo muda wake wa kuwa Chelsea unaweza kuisha mapema zaidi kuliko watu wanavyoamini.m

No comments:

Post a Comment