TAARIFA KWA UMMA: LIPULI YAKANUSHA KUFUKUZWA KWA MALIMI BISUNGU NA MACHAKU SULUM , KINACHOENDELEA NDANI YA CLUB HIKI APA>>>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Friday, November 3, 2017

TAARIFA KWA UMMA: LIPULI YAKANUSHA KUFUKUZWA KWA MALIMI BISUNGU NA MACHAKU SULUM , KINACHOENDELEA NDANI YA CLUB HIKI APA>>>>




TAARIFA KWA UMMA
Uongozi wa LIPULI FC unapenda kuchukua fursa hii kukafnusha taarifa zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu wachezaji Malimi Busungu na Machaku Salum Machaku ambao wameripotiwa kufukuzwa na timu kwa tuhuma za ulevi uliopindukia.
Uongozi unakanusha vikali taarifa hizo na badala yake sasa unatoa ufafanuzi juu ya wachezaji hao.
Wachezaji Malimi Busungu na Machaku Salum Machaku hawajafukuzwa ila wamesimamishwa kwa muda kwa makosa ya kinidhamu na suala lao kwa sasa linafanyiwa kazi na Kamati Tendaji kwa ushirikiano na Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi.
Kwa sasa itoshe kusema wachezaji hao bado ni mali ya LIPULI FC na taarifa rasmi juu ya hatma yao itatolewa baada ya kikao cha Kamati Tendaji na Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi kitachofanyika siku ya jumapili tarehe 5 ya mwezi huu.

Imetolewa na Clement Sanga-Msemaji LIPULI FC.

No comments:

Post a Comment