HAJI MANARA AWASHAMBULIA WACHEZAJI SIMBA>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Thursday, November 30, 2017

HAJI MANARA AWASHAMBULIA WACHEZAJI SIMBA>>

TATIZO  LA SIMBA NI UCHEZAJI WA WACHEZAJI NA SIYO WAAMUZI Haji Manara.

Mimi ni shabiki wa simba nitimu ambayo nimeipenda na imenisababishia shuruba nyingi utotoni.Nimekula viboko,Nikiwa na miaka sita Tuu  kwa kosa la kuweza kupanga kikosi kamili cha simba pamoja na wachezaji wa akiba lakini nashindwa kukariri "Orodha" na kumbuka sana licha ya Viboko vile sikuwahi kupunguza Mapenzi kwa timu hii.Kila mechi ilipofika niliwahi kuchemsha Betri na kuzianika juani tayari kuhimili mikiki ya redio yetu ya NATIONAL soma nationali

Tatizo la Simba ni wachezaji kucheza kinazi na kukosa ari ya kutafuta ushindi wana ridhika haraka kwa kujiona wachezaji bora na wana kiwango cha juu wa kati uhalisia sio huo.Washambuliaji wa simba ni washambuliaji wanaoridhika haraka kuliko washambuliaji wa Timu zote katika Ligi Kuu

Nikweli Kuna mazingira Yanga wana Bebwa lakini uzuri wa Yanga ukiwabeba wanabebeka. Washambuliaji wake hawaridhiki...wana kiu ya ushindi...wana hasira ya ushindi...unaona kabisa hawataki kuwaangusha mashabiki wao hali haiko hivyo kwa simba?! Simba wachezaji wetu hawana nidhamu uwanjani hawajitumi ipasavyo ,ni wazito ,hawajali hisia za mashabiki zao wanacheza kwa kiburi na majivuno na hii inatokana na kelele kama hizi za Haji Manara za kuto kusema Ukweli.

Namna Pekee ya kufanya  SIMBA iwajibike ni kuhakikisha kunakuwa na wasambuliaji wenye kiu ...Ni wakati wa  Omogo kufanya maamuzi Magumu kuna haja gani ya kuweka wachezaji wazuri Benchi kama  kijana Mohamed Ibrahim na kung`ang`aniza Mshambuliaji kama Mavugo ambaye anaingia kwa hali ya uchovu na kucheza kichovu muda wote kama amelazimishwa?! .Nauliza tu si ingilii kazi ya Ukocha.

Mechi na Lipuli tutamlaumuje Refa ambaye alituokoa ?! Hivi kama hata Refa huyu tunamlaumu ni refa Yupi tutampongeza?! Manara na Kauli zenu za Kizembe na Uvivu wa wachezaji wa Simba  Mnatuumiza sana mashabiki na kutupa wakati Mgumu sana.Wachezaji ni tatizo kubwa siyo MAREFA.

No comments:

Post a Comment