Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga ambao awali ulipangwa kuchezwa Aprili 7, mwaka huu, tayari baadhi ya wachezaji wa timu hizo hawataweza kucheza kutokana na sababu mbalimbali.
Katika msimamo wa ligi hiyo, timu hizo kwa sasa zinatofautiana mabao ya kufunga lakini zikiwa sawa pointi kwa pointi 46, Simba ipo kileleni ikifuatiwa na Yanga ingawa Simba wana mchezo mmoja mkononi.
Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliopigwa Oktoba 28, mwaka jana ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, vikosi vilivyoanza vya timu hizo mbili ni tofauti na vile ambavyo vinatarajiwa kukutana mwezi ujao.
Kuelekea mchezo huo, kwa upande wa Simba wachezaji ambao watakuwa wapya ambao kwa sasa wamekuwa wakicheza kikosi cha kwanza ni Asante Kwasi, Nicholaus Gyan, Shomari Kapombe, Jonas Mkude na John Bocco ambao wote hawakucheza mchezo wa kwanza.
Ambao wameondolewa kwenye kikosi ni Mohamed Ibrahim ‘Mo’, Method Mwanjale, Haruna Niyonzima, Mzamiru Yassin na Laudit Mavugo, ukiachana na Mwanjale ambaye ameachwa, wengine ni wagonjwa na wengine hawana nafasi kikosi cha kwanza.
Kwa matangazo usisite ututafuta kwenye email yetu
nisphory@spoti.co.tz

No comments:
Post a Comment