DIFAA EL JADIDI YA MSUVA USO KWA USO NA TP MAZEMBA NI BAADA YA DROO YA LIGI YA MABINGWA AFRICA>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Thursday, March 22, 2018

DIFAA EL JADIDI YA MSUVA USO KWA USO NA TP MAZEMBA NI BAADA YA DROO YA LIGI YA MABINGWA AFRICA>>

Timu ya mshambualiaji wa kimataifa wa Tanzania Simon HappyGod Msuva Difaa El Jadidi imepangwa katika kundi B la ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Difaa El Jadidi ipo Kundi moja pamoja na timu za MC Alger, TP Mazembe ambao ndio mabingwa wa kombe la Shirikisho Barani Afrika na ES Setif.

Mechi za kwanza za kundi hilo zitafanyika Mei 5 ambapo timu mbili zitakazoongoza kundi zitaingia katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa Kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

Simon Msuva ambaye mpaka sasa amefunga mabao manne kwenye michuano hiyo anatakiwa kuiongoza timu yake kutwaa taji hilo ili iweze kujishindia zawadi ya kombe la dola Milioni 2.5 za kimarekani.

Kundi A

1. Al Ahly (Misri)

2. Township Roller (Botswana)

3. KCCA (Uganda)

4. Esperance (Tunisia)

Kundi B

1. Difaa El Jadidi (Morocco)

2. MC Alger (Algeria)

3. ES Setif (Algeria)

4. TP Mazembe (DR Congo)

Kundi C

1. AS Port (Togo)

2. Horoya (Guinea)

3. Mamelodi Sundowns (South Africa)

4. Wydad Casablanca (Morocco).

Kundi D

1. Zesco United (Zambia)

2. Primeiro de Agosto (Angola)

3. Etoile du Sahel (Tunisia)

4. Mbabane Swallows (Swaziland)

No comments:

Post a Comment