Mshambuliaji Obrey Chirwa wa Yanga amefikisha mabao 10 mbele ya mshambuliaji na nahodha wa Simba, John Bocco.
Bocco ana mabao tisa ya kufunga katika Ligi Kuu Bara, Chirwa naye amezidisha idadi hiyo leo.
Chirwa amefunga mabao matatu katika mechi dhidi ya Njombe mji ambayo inaendelea kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Katika mechi hiyo, Chirwa alipachika mabao matatu na moja likawekwa kimiani na Emmanuel Martin.
No comments:
Post a Comment