|
Mshambuliaji nyota wa Difaa al Jadida ya Morocco, Simon Msuva ametua nchini kwa ajili ya mapumziko na kusema atapambana hadi apate nafasi ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.
Msuva amesema viwango vya Tanzania katika Fifa ni sehemu ya kikwazo lakini hatakubali kushindwa.
“Naendelea kupambana ili nifikie ndoto yangu ya kucheza Ulaya, nataka kufika huko lakini viwango vyetu vya Fifa bado. Lakini nitaendelea kupambana,” alisema.
Alisema amerejea nyumbani kwa ajili ya mapumziko ya wiki moja na nusu na atautumia muda huo kuwa karibu na familia yake.
No comments:
Post a Comment