Manchester United wanataka kumrudisha mlinzi Jonny Evans Old Trafford, miaka miwili unusu baada ya kumuuza mchezaji huyo wa miaka 29 kwenda West Brom,
Mourinho amesema ilikua ni kosa kubwa sana kwa mwalimu wa zamani wa Manchester United Van Gaal, kumuuza mlinzi huyo wa kati kwa pauni milioni 6.
Hivi sasa Manchester United wamejiandaa kutoa pauni 30milioni ili waweze kumtwaa Captain wa Brom Evans mwenye miaka 29.
Man City walionyesha nia ya kutaka kumsaini Mlinzi huyo msimu uliopita lakini walishindwa (Sunday Mirror)
Juventus wanaonekana kuwa na nia ya kumuuza mlinzi Alex Sandro lakini Chelsea walioshindwa kumsaini mbrazil huyo msimu huu, wanakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City, Manchester United na Paris St-Germain. (Sunday Express)
Daniel Sturridge ameambiwa anaweza kuondoka Liverpool kwa mkopo mwezi ujao na meneja Jurgen Klopp wakati mchezaji huyo wa miaka 28 raia wa England anataka kujitafutia nafasi katika kombe la dunia (Sun on Sunday)
Meneja wa Liverpool anasema kuwa alishinikizwa na maajenti wake kumsaini Mohamed Salah msimu huu baada ya hofu kuwa wing'a huyo wa Misri wa umri wa miaka 25 alikuwa mdogo sana kuweza kufanikiwa katika Premier League. (Mail on Sunday)
Manchester United wanatathmini ikiwa watatoa ofa ya karibu milioni 30 kwa wing'a wa Bordeaux mbrazil Malcom, 20, mwezi Januari.(Sunday Times)
Manchester City wamemtazama mlinzi wa Augsburg mjerumani Philipp Max, 24, wakati wanataka kujaza nafasi ya mfaransa aliye na jeraha Benjamin Mendy. (Mail on Sunday)
Meneja wa Everton Sam Allardyce analenga kumsaini mshambuliaji wa Crystal Palace mBelgiji Christian Benteke, 27, wakati wa msimu mpya wa kusaini wachezaji wapya mwezi ujao. (Sunday Mirror)
No comments:
Post a Comment