TAMBWE APIGA HESABU NDEFU KUMNG'OA OKWI >>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Friday, December 29, 2017

TAMBWE APIGA HESABU NDEFU KUMNG'OA OKWI >>>

Straika wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe amemtaka Mganda wa Simba, Emmanuel Okwi kukaa sawa katika vita ya kuwania tuzo ya ufungaji bora msimu huu kwani yeye kazi hiyo anaianza Jumapili hii katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbao FC.

Tambwe ambaye ni mshindi mara mbili wa tuzo hiyo tangu atue hapa nchini msimu wa 2013/14 amesema kuwa licha ya kuwa nyuma ya Okwi kwa mabao nane lakini anaamini kuwa ana uwezo wa kumfikia na kumuacha ndani ya mechi sita.

Straika huyo amesisitiza kuwa ana uchu mkubwa wa kutaka kuandika rekodi mpya msimu huu ya kuibuka mfungaji bora, kwa hiyo Okwi pamoja na wachezaji wengine wote wanaochuana kuwania tuzo hiyo wajipange.

“Furaha yangu siku zote huwa ni kufunga, huwa sijisikii vizuri kama nitamaliza mechi bila kufunga hata bao moja.

“Hivi sasa nimepona na nipo fiti, kwa hiyo nataka kuandika rekodi nyingine ligi kuu katika mechi 19 za ligi kuu zilizobakia kwa timu yetu.

“Pia endapo mambo yatakaa sawa, nataka nitumie mechi sita tu kumfikia Okwi, kwa hiyo akae mkao wa kula, Mungu akipenda kazi hiyo nitaianza Jumapili hii dhidi ya Mbao FC,” alisema Tambwe.

No comments:

Post a Comment