SIMBA WAANZA JEURI , WAJILINGANISHA NA TP MAZEMBE>>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Monday, December 4, 2017

SIMBA WAANZA JEURI , WAJILINGANISHA NA TP MAZEMBE>>>

Jiunge nasi kila siku kwa habari mbali mbali.   KASULUWADAU. SPORTBLOG.COM

HII NDIO SIMBA BUANAAAAA……
Kwa Tanzania, Simba ndio kila kitu na inaanzisha kila jambo na kuigwa na wengine…
 Ukifatilia utaona mambo mengi yanaanzishwa na Simba kwa  mpangilio na wengine wanaiga kwa kukurupuka.
 Hata lilipotolewa wazo la kuingia katika hisa, wenzetu wakakurupuka na kutaka kukodidha kabisa timu kwa miaka kumi!!!!
 Ndio maana jana waziri Mwakyembe akasema wasione aibu kuiga kizuri…….
 Nitakupa dondoo ya mambo machache ambayo Simba walikua wa kwanza kuyafanya Tanzania…
1.
Simba ndiyo timu ya kwanza nchini kupanda ndege na hii ilikuwa mwaka 1963 tena wakati huo taifa la Tanzania halikuwa limeundwa, ilikwenda Ethiopia kwa mwaliko wa rais wa taifa hilo Haile Selassie
2. Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa jezi na hii ilikuwa 1938 ilipocheza na kombaini ya mabaharia wa meli zilizotia nanga kwenye bandari ya Dar es salaam.
3. Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa viatu nchini na hii ilikuwa1949 ilipocheza na kombaini ya jeshi la majini Navy ya Afrika Kusini.
4. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa na basi lake yenyewe na hili lilinuliwa mwaka1968.
5. Simba ndiyo timu ya kwanza kumiliki jengo lake lenyewe na hili lilizinduliwa 1971.
6. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa bingwa wa ligi kuu nchini1966.
7. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwakilisha nchi na hii ilikuwa 1967.
8. Simba klabu ya kwanza nchini kwenda Ulaya na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland
9. Simba ndiyo timu ya kwanza kuwa mabingwa wa Afrika Mashariki na kati na hii ilikuwa 1974.
10. Simba ndio mabingwa wa kihistoria wa Afrika Mashariki na Kati, ndiyo timu iliyochukua ubingwa mara nyingi kuliko klabu yeyote Afrika Mashariki na Kati (Champs off all time.)
11. Simba ndiyo timu pekee nchini iliyowahi kufika nusu fainali ya klabu bingwa Afrika na hii ilikuwa1974.
12. Simba ndiyo timu pekee nchini na Afrika Mashariki kufika fainali ya kombe la Caf na hii ilikuwa1993.
13. Simba ndio timu inayoshikilia rekodi Afrika kama si duniani kwa kufungwa na Mufurila Wonderers ya Zambia magoli 4-0 na kwenda kuibamiza 5-0 kwao, mbele ya rais wao Kenneth Kaunda. Hii haijafanywa na klabu yeyote Afrika na nina mashaka duniani, hii ilikuwa 1979.
14. Simba ilicheza katik hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika 2003 kwa mafanikio makubwa kulinganisha na timu yoyote nchini.
15. Simba ndiyo timu pekee kuivua ubingwa klabu bingwa Afrika nadi Zamalek hii ilikuwa pia 2003.
16. Simba ndiyo klabu pekee nchini kuzifunga timu zote za mataifa ya kiarabu kuanzia
• Waliowatoa mwaka jana Etoile du Sahel (Tunisia)
• Widad Casablanca (Morocco)
• El Setif (Algeria)
• El Harach (Algeria)
halaf tumezifunga timu zote kubwa za Misri Zamelek,Al Ahly, Arab Contractors, Ismailia, Mehala, Al kubra na timu nyingine mnajua huwa inafanywaje ikigusa kule.
Pia imeshaitoa El Merekh ya Sudan 1994 katak klabu bingwa ya Afrika. Simba pia imeshazifunga miamba ya Afrika Magharibi kuanzia Asec, Asante Kotoko, Hafia ya Guinea hata mabingwa wa kihistoria wa Zambia Nkana Red Devils.
17. Tukirudi juu Simba ndiyo timu ya kwanza kuvaa suti na hii ilikuwa 1974 ilipokwenda Poland.
18. Simba ndiyo klabu pekee nchini kujenga jengo lake yenyewe kwa nguvu za wanachama na mashabiki, wenzetu ni mkopo na msaada toka kwa mzee Karume100%, Simba ilipewa kiasi flan na mzee karume baada ya jengo kukamilika na hii ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 70.
18. Na sasa Simba ndio wa kwanza kuinga katika umiliki wa Hisa……. Ukiondoa hizi timu zinazosema zina hisa lakini  mmiliki anakua mmoja au hata mpangilio haueleweki…..
 HII NDIO SIMBA BUANAAA

No comments:

Post a Comment