Beki kiraka wa Simba, Asante Kwasi anaonekana hataki utani hata kidogo maana tokea ametua jijini Dar es Salaam ameendelea kujifua mfululizo bila kuchoka.
Kwasi raia wa Ghana alianza mazoezi leo asubuhi katika ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.
Lakini ameendelea na mazoezi hayo makali leo jioni akionyesha wazi amepania kupata fitnesi ya kutosha kabla ya kujiunga na Simba na kuanza kazi.
Simba imemuongeza Kwasi kuchukua nafasi ya Method Mwanjali, beki mkongwe kutoka Zimbabwe ambaye alikuwa tegemeo la safu ya ulinzi kabla ya kuanza kuandamwa na majeraha.
No comments:
Post a Comment