DJUMA MASOUD KOCHA SIMBA , ASEMA TIMU YAKE IKO FITI NA AMEELEZA HAYA>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Thursday, December 28, 2017

DJUMA MASOUD KOCHA SIMBA , ASEMA TIMU YAKE IKO FITI NA AMEELEZA HAYA>>

Kaimu Kocha Mkuu wa Simba, Masoud Djuma ameweka msimamo wake kuwa kikosi chake kitacheza kwa ushirikiano na hakutakuwa na staa mkubwa kuliko timu.

Djuma ambaye anashikilia nafasi ya kocha mkuu baada ya kufutwa kazi kwa Joseph Omog, amesema anapambana kuhakikisha kikosi chake kinafanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wake lakini hatataka kuona kuna makundi.

“Kuwa na wachezaji ambao ni muhimu zaidi ya wenzao, hili si jambo jema. Hakutakuwa na mambo hayo na zaidi ningependa ushirikiano na upendo.

“Hii timu ni yetu sote, lazima kuwe na ushirikiano kuhakikisha tunafikia lengo na ndilo lengo la kila mmoja wetu,” alisema.


Kocha huyo raia wa Burundi, ametokea Rayon Sports ya Rwanda ambayo alifanikiwa kuopa makombe mawili ya ubingwa wa ligi na Kombe la Amani kama Kombe la Shirikisho hapa nyumbani

No comments:

Post a Comment