SIMBA SASA KAZI IPO , NDANDA WASHINDA MAZOEZINI KUHAKIKISHA HILI LINAWAKUTA SIMBA>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Monday, December 25, 2017

SIMBA SASA KAZI IPO , NDANDA WASHINDA MAZOEZINI KUHAKIKISHA HILI LINAWAKUTA SIMBA>>

Kikosi cha Ndanda FC kinaonekana hakitaki mchezo katika mechi yake ijayo dhidi ya Simba ambao sasa hawana kombe lolote mkononi.

Benchi lake la Ufundi la Ndanda FC chini ya kocha wake mkuu, Malale Hamsini, linajipanga kuhakikisha timu yao hiyo inaibuka na ushindi dhidi ya Simba baada ya kuamua kwenda ufukweni kujinoa zaidi.

Ndanda ambayo hivi sasa ipo nafasi ya 11 kwenye Ligi Kuu Bara, Jumamosi ijayo itapambana na Simba kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara ukiwa ni mwendelezo wa ligi hiyo.

Kocha huyo alisema juzi Jumamosi walifanya mazoezi hayo ya ufukweni katika Ufukwe wa Msemo uliopo Mtwara ili kuongeza stamina kwa wachezaji.

“Tunajiandaa vizuri kuhakikisha pointi tatu zinabaki nyumbani hiyo Jumamosi tutakapocheza na Simba katika uwanja wetu wa nyumbani.


“Katika kujiandaa huko, tumeamua kufanya mazoezi ya ufukweni ili kuongeza stamina kwa wachezaji, kikubwa tunazihitaji sana hizo pointi ili tuzidi kupaa kutoka kwenye nafasi tuliyopo sasa,” alisema Hamsini.

No comments:

Post a Comment