MAKALA FUPI : WANA SIMBA HAKUNA SIMBA BILA MAPAMBANO YA WACHEZAJI , ASANTE MO DEWJI>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Monday, December 25, 2017

MAKALA FUPI : WANA SIMBA HAKUNA SIMBA BILA MAPAMBANO YA WACHEZAJI , ASANTE MO DEWJI>>

HAKUNA MAAJABU ZAIDI KAMA HUJUI THAMANI YA JEZI YAKO..
..
..
..
Ulipofika msimu wa 2007 kocha Jose Morinho aliaondoka Chelsea na baadae alikwenda kujiunga na Internazitionale Milano au Inter Milan...Jose Morinho alipofika tu Inter Milan Alianza kumwaga sumu kwa kikosi hiko alisema saana na wachezaji wake aliwajaza maneno mengi tu...aliwaambia Diego Milito na Mario Ballotelli Nyinyi mna uwezo mkubwa saana wakuziona nyavu kama ilivyo kwa Lionel Messi au Cristiano Rinaldo...Morinho aliendeerea kuzungumza zaidi alizungumza na Thiago Motta Pamoja na Wesley Snejder kwamba mnaweza kuliwatara dimba kama ilivyo kwa Xavi Hernandez Na Andres Iniesta...Alienderea Kuwajaza maneno wakiongozwa na Nahodha Zanneti wakati ule hivi unafikiri Jose Morinho alikuwa mjinga? Hapana Morinho aliitaji Inter Milan ijitume hakukuwa na maajabu mengine zaidi ya kujituma tu...mwisho was Siku utimamu wa Jose Morinho ulionekana ardhi ya San Siro ikawa yamoto saana...na may 22 Kupitia kwenye mguu wa Diego Milito Inter Milan waliiangamiza Bayern Munich Ya Louis Van Gaal Pale Santiago Bernabeu katika fainali ya Uefa Champions League....Tena Walikamilisha Treble Yani walishinda makombe matatu Serial A,Coppa Italy Pamoja Na Uefa Champions League Msimu Huo Huo Wa 2010....Umeona Utimamu wa Morinho? Silaha kubwa Inter Milan waliamua kujituma saana ukiachilia mbali maneno ya Morinho..
..
..
..
Hivi inawezekana kweli team kama Moro United kupanda Ligi kuu Tanzania bara na kuchukua kombe hilo msimu Huo Huo? Jibu litakuwa hapana inaweza kuwa rahisi kwa Ben Pol Kufanya collaboration na John Legend...Lakini Si Moro united kupanda Ligi kuu na kuchukua kombe tumeona kwa Toto African ambao wamepanda lakini hawakuwa na pumzi ya kutosha hatimaye tukawapa mkono wa kwaheri na kurudi walikotoka....Cha Ajabu sasa kuna Team Ilipanda daraja na kuingia Ligi kuu ya England na kuchukua kombe ajabu eeeh! Hivi nani anaikumbuka Leicester City ilotwaa ubingwa Pale England? Ndio hao hao walipanda Ligi kuu na kuwa mabingwa...Kwanini isiwe arsenal,Chelsea Au Liverpool? Leicester City walipogundua thamani ya jezi zao wakaona kwanini wasipambane na kuifanya ardhi ya King Power kuwa na maumivu kwa kila atakae itembelea...Basi wakafanikiwa wao hawakuwa Na David De Gea Ila walikuwa na Kasper Peter Schmeichel...Hawakuwa Na Nemanja Matic wao walikuwa na N'Golo Kante wao...Hawakuwa hata na David Silva walikuwa na Shinji Okazaki wao...Lakini bado walitesa na Striker wao Jimmy Vardy Alimaliza Nafasi ya Pili akiwa kama Top Score Wa EPL tena kwa tofauti ya goli moja nyuma ya Harry Kane...hata Riyard Mahrez wao alifunga Goli 17 mwisho wa Sikh Leicester City wakiongozwa na Claudio Raniera walitangazwa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Ya England Lakini yote kwa sababu walipigana na walijua thamani ya jezi zao...umejifunza kitu hapo??
...
...
...
HAKUNA SIMBA SC CLUB BILA MAPAMBANO YA WACHEZAJI...
...
...
...Joseph Omong tayari ametimuliwa saawa pengine hakuona thamani ya miguu ya Mohammed Ibrahim,Nikolas Gyan na Said Ndemla...muda mwingi alikariri alikuwa anawaza kuhusu Mzamiru Yassin Na Haruna Niyonzima Ndio Huyo huyo Joseph Omong alikuwa akiona Jonas Mkude Asingeweza Kumsaidi saana katika midfielder... Sitaki kuzungumza kuhusu Joseph Omong Nataka Nizungumze Kuhusu Simba Na Wachezaji Kwaujumla....Silaha Ya Inter Milan Na Leicester City Nilizo Zizungumzia Halo Juu Wala Hakuna Tofauti Saana....
...
...
...
Nilikuwa nautazama vyema mchezo wa Simba Vs Green Warriors hahaha inachekesha saana sikuona ile Fighting Spirts(roho ya upambanaji) ifike mahara wachezaji wa Simba Wajue tupo hapa kwaajiri ya Simba tunatakiwa kujituma saana tena kujituma haswaa kaajiri ya kutafuta ubingwa Simba Hakuna kitu inachoitaji kwa sasa zaidi ya ubingwa sasa nani atawapa ubingwa? Wachezaji wanatakiwa kupambana kwa jasho na damu...ufike muda ambao tukose kujua tofauti ya Tshabalala na Jamal Mwambeleko kutokana na mapambano wachezaji wetu wasivae jezi tu...jezi bila kupambana sikitu...Lazima wajue thamani zao na Simba Kwaujumla watambue kwanini wapo Simba...
...
...
...
Hivi ulishawahi kumshuhudia Haruna Moshi Boban? Au hata Juma Nyosso....Na ni nani anaikumbuka ile Simba Unbeaten? Ndio naizungumzia Simba ambayo ilimaliza Ligi Tanzania bara bila kufungwa? Simba ambayo ilijawa na wanaume sio wavulana Simba ile haina tofauti na hii isipokuwa wachezaji wanataka kujivunia kuwa Simba bila kufahamu kwanini wapo Simba....Simba Ile ambayo iliweza kuisumbua Tp Mazembe ya LAMINE N'DIAYA kwenye ubora wake...Wapambanaji kama Patrick Mafisango(R.I.p) Musa Hassan Mgosi....Watu ambao waliweza kuwasumbua kina Given Singuruma,Rainford Kalaba,Nihayo Kazembe...Lakini Leo Hii Simba Inatolewa Na Green Warriors? Team kutoka Daraja LA Pili...Mbali na uzembe wa kocha mchawi namba moja ni uvivu...nikiwa na maana mapambano ni muhimu wachezaji wajue umuhimu wao...jasho liwatokalo liwe lauchungu kuu ya Simba..
..
..
..Inamaana Hawakuwai Kuona Bastian Schweinsteiger Na Bayern Munich Yake...Au Frank Lamapard Na Chelsea Yake...Au Steven Gerrard Na Liverpool Yake...Au Paul Choles Na United Yake...Inamaana Hata Puyol Na Barcelona Yake Hawakumuona?..
...
...
...
Mpira ni mapambano lazima Simba wawe makini...kila mchezaji ajue kwanini yupo Simba ndio maana nikasema...HAKUNA MAAJABU KAMA HUJUI THAMANI YA JEZI YAKO....
....Kuandika saana inaweza kuwa moja kati 

No comments:

Post a Comment