NGASA AWATOA HOFU WANA YANGA , ASEMA SIMBA ATAPIGWA IDADI HII YA MAGOLI>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Saturday, December 30, 2017

NGASA AWATOA HOFU WANA YANGA , ASEMA SIMBA ATAPIGWA IDADI HII YA MAGOLI>>

Jumamosi ya wiki hii, Simba itakuwa uwanjani kupepetana na Ndanda FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, wakiwa mkoani Mtwara, Simba wanatarajiwa kukutana uso kwa uso na Mrisho Ngassa anayeichezea Ndanda kwa sasa.
Ngassa amesajiliwa Ndanda hivi karibuni akitokea Mbeya City ya Mbeya na anatarajiwa kuongoza mashambulizi ya kuivaa Simba katika mchezo huo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Jumamosi hii.
Kocha wa Ndanda FC, Malale Hamisi amedai kuwa Mrisho Ngassa anatarajiwa kuwa msaada mkubwa kwao na anaamini uwepo wake utawasumbua Simba katika mchezo wao.
Kocha Mahale amesema maandalizi yao yanaendelea vizuri pia uwepo wao nyumbani unawapa nguvu kubwa ya kupambana na kuhakikisha wanawasumbua Simba.
Ameongeza kuwa wale wanaoamini Ngassa amekwisha kiuwezo uwanjani, watashangaa kitakachotokea katika mchezo huo.
Anaamini Ngassa kwa sasa ameifanya Ndanda kuwa tofauti na uzoefu wake utawasaidia katika mchakato wa kuzitafuta pointi tatu za mtanange huo wa Ligi Kuu ya Vodacom

No comments:

Post a Comment