Ajibu aipa Yanga SC Ushindi wa 4G dhidi ya Stendi Stand United. - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Friday, October 27, 2017

Ajibu aipa Yanga SC Ushindi wa 4G dhidi ya Stendi Stand United.


Mchezaji Ibrahim Ajib ameendelea kuwasha moto akiwa na Timu yake ya Yanga SC baada ya leo Jumapili October 22, 2017 kuifungia mabao mawili Timu yake kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Stand United na kuifanya Yanga SC ifikishe pointi 15 sawa na Simba SC na Mtibwa Sugar. Simba SC na Mtibwa Sugar zilifikisha alama 15 baafa ya kushinda michezo yao ya jana kwa Simba SC 4-0 dhidi ya Njombe Mji FC lakini ushindi wa Yanga SC leo unafanya timu tatu kufungana pointi lakini tofauti ya magoli ndio unazitofautisha katika msimamo wa ligi. Ajib ndio anaongoza kwa ufungaji kwenye kikosi cha Yanga akiwa na magoli matano (5) aliyoyafunga kwenye mechi saba alizocheza. Ajibu yupo nyuma ya Emanuel Okwi kwenye orodha ya wafungaji VPL 2017/2018, Okwi amefunga magoli nane (8), Ajib magoli matano (5) na Mohamed Rashid wa Tanzania Prisons mwenye magoli manne (4). Yanga SC ilikuwa haijashinda mechi kwa zaidi ya magoli mawili, huu ni ushindi wao mkubwa Tangu kuanza kwa VPL msimu huu. Walifunga goli moja mfululizo kwenye mechi zao nne za kwanza kabla ya kupata ushindi wa magoli 2-1 walipocheza dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliopita.

No comments:

Post a Comment