MUZAMIRU YASSIN MASHART MAGUMU SIMBA>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Sunday, December 3, 2017

MUZAMIRU YASSIN MASHART MAGUMU SIMBA>>

atika tetesi za hivi karibuni zinasema Klabu ya Al Rustaq ya Oman ndiyo imeanza kufanya mazungumzo na Simba, lakini yakaishia juu kwa juu kwa viongozi, ingawa Mzamiru alishtukia swala hilo.

Hata hivyo baada ya waandishi kumuoji alifunguka haya.... "Bado nina mkataba wa miezi sita na Simba, ila ukimalizika tu klabu inayohitaji huduma yangu, iwe na Milioni 70, ininunulie gari pamoja na kunipangia nyumba ya kuishi, kuhusu mshahara ni makubaliano ya siri baina yangu na wahusika,”

Pia aliongezea kwa kusema “Hata klabu yangu ya Simba ikiwa na dau hilo nitakuwa tayari kuitumikia, kwani soka kwangu ni kazi ambayo nimeichagua kwa ajili ya kuendesha maisha yangu,”.

Mzamiru alisema licha ya kubakiza miezi sita Simba, ataendelea kujituma kwa bidii na kuongeza ushindani katika namba yake na hamu yake kubwa ni kuona klabu hiyo inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

“Natamani kuwa mmoja wa wale ambao watachukua ubingwa wa ligi ndani ya kikosi cha Simba, msimu uliopita tulichukua Kombe la FA na hivyo tumeanza kazi ya kurejesha vikombe klabuni kwetu,” alisema Mzamiru aliyeibukia kuwa kipenzi cha mashabiki. Katika fainali ya FA Simba iliibuka kidedea kwa kuifunga Mbao FC mabao 2-1.

No comments:

Post a Comment