MAKALA : SIMBA NA YANGA KWA KAURI HIZI HAMTAFIKA POPOTE KISOKA>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Wednesday, December 13, 2017

MAKALA : SIMBA NA YANGA KWA KAURI HIZI HAMTAFIKA POPOTE KISOKA>>

Habari msomaji wetu wa ukurasa huu wa KASULUWADAU ni matumaini yangu u mzima wa afya , Binafsi tu tunashukuru Mungu mwingi wa rehema kutuwezesha kufikia siku kama ya leo,

Shukrani zangu za dhati ziende kwa fundi mitambo wetu Alexander Vyankende ambae yeye ndie anatufanya tupatikane hewani kila kukicha katika ukurasa wetu huu pendwa kabisa.

Lakini pia usikose kutembelea ukurasa huu kila mara kwani ndio page pekee inayokuletea mambo mengi mapya kila kukicha tukianza na habari za Magazeti kila alfajili na kufuatia habari mbali mbali za makala na michezo.

Habari yenyewe ambayo nimeona niizungumzie muda huu ni kuhusiana na ushabiki usio na tija kwa mashabiki wa timu mahasimu za simba na yanga,

Kwa mfano unajifunza nini unapoandika kashifa inayomuhusu mtu flani na kuipablish , binafsi sijapenda na naomba niiweke hii wazi ili mashabiki tujilekebishe kwa hili

Habari yenyewe hii hapa

ITAMCHUKUA MWANA YANGA MUDA MREFU KUWEZA KUMSIFU IBRA_AJIBU.

Wazungu husema enough is enough.
Mashabiki wa kandambili wamekuwa wakiharibu wachezaji wa bongo,hivi tumewahi tena kumsikia HASSAN KESSY??
Huwezi kumsikia tena kwa kuwa kule YANGA matokeo ya timu hayatokani na jitihada za uwanjani wala mipango na mikakati Bali mbinu za nje ya uwanja.

Yanga wameweza kuchukua ubingwa kwa kuwakojoza wachezaji na hata viongozi wa timu zisizo na #umatemate.
Huku wachambuzi wa soka wakikiri kwamba soka LA Tanzania limeendelea kushuka,mashabiki wa yanga wameendelea kuwasifu wachezaji wa timu yao na kufika hatua ya kusema goli LA AJIBU lina THAMANI ya milioni 40,huu ni ujinga kwa kumsifia mchezaji uliemsajili kwa pesa kubwa ya uhamisho,unamlipa mshahara usiopungua milioni 3 kwa mwezi kisha unaihonga timu anayokwenda kucheza nayo ili ikubali kushindwa kwa kuahidiwa PESA.

AJIBU kama mchezaji mkubwa zaidi wa tanzania katika michuano ya CECAFA anacheza kwa kiwango cha chini na kushindwa kuibeba Kilimanjaro stars,

Mashabiki ngerengere wa YANGA ndio wanaoongoza kelele za kusema tatizo liko kwa kocha wa Kilimanjaro stars na wala sio wachezaji.

UKWELI UTABAKI UKWELI

YANGA MNAHARIBU SOKA LETU KWA KUHONGA VIJANA.

No comments:

Post a Comment