TFF YAITUMIA SIMBA BARUA*
Shirikisho la Soka Tanzania Tff limetuma Barua kwa Klabu ya Simba Sc baada ya kauli ya Afisa Habari na mawasiliano wa Klabu hiyo Haji Manara ambazo kwa Mujibu wa Tff ni tuhuma dhidi ya Waamuzi.
Manara aliitisha Mkutano na Waandishi wa Habari siku ya Jana katika makkao makuu ya Klabu hiyo yaliyopo Msimbazi jijini Dar es salaam, Manara alizungumzia masuala mbalimbali ikiwemo suala la Mwamuzi aliyechezesha pambano kati ya Simba na Yanga siku ya Jumamosi ambapo kwa mujibu wa Manara alikuwa na Makosa mengi ikiwemo kuwanyima penati Simba.
Afisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania Alfred Lucas Mapunda amezungumza na waandishi wa kueleza kuwa tayari shirikisho hilo limetuma barua kwa Simba kutaka kujua kusudio lao huku pia wakihitaji Maelezo ya kina kutoka kwa Haji Manara nini lengo lake kutoa kauli hizo ambazo TFF inaona ni uchochezi na uvunjifu wa sheria
No comments:
Post a Comment