Katika kile ambacho kinaonekana kuwa hali ya mambo kwa beki wa kulia Shomari Kapombe siyo nzuri, kuna tamko limetolewa kuwa kuna uwezekano mkubwa mchezaji huyo akatemwa katika dirisha dogo la usajili linalotarajiwa kufunguliwa November 15 keshokutwa.
Kapombe alisajiliwa na Simba akitokea Azam FC lakini tangu atue klabuni hapo ameshindwa kupata nafasi ya kucheza muda mrefu kutokana na kuandamwa na majeraha ya muda mrefu.
Katika kile kinachoonekana wazi mchezaji huyo ataondolewa klabuni hapo, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans oppe amenukuliwa akisema kuwa Kapombe anatakiwa kucheza kama anaona afya yake haipo sawa ni vema akakaa pembeni ili akipona arejeshwe kikosini.
Akifafanua zaidi, Hans Poppe alisema: “Vipimo havidanganyi, yeye kama anaona hawezi kucheza basi akae pembeni, siyo anakaa anakula mshahara wa bure. “Kama amepona acheze, kama hataki basi aondoke, majeruhi gani ambaye haponi muda wote huo.” Alipoulizwa kuhusu vipimo vinavyosema, alisema: “Vipimo vinaonyesha ameshapona vizuri, yeye ana uwoga wake, labda anaogopa ataumia, msimamo wetu ni yeye mwenyewe aamue acheze au achezi.” Ikumbukwe kuwa akiwa Azam FC, Kapombe alikuwa akipatiwa matibabu mara kwa mara kwa kupelekwa nchini Afrika Kusini, alipopona alirejea uwanjani na kuitumikia timu hiyo kama kawaida.

No comments:
Post a Comment