HOFU KUHUSU IMANI YA MSALABA - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Tuesday, November 14, 2017

HOFU KUHUSU IMANI YA MSALABA

IJUE MAANA YA ISHARA YA MSALABA.

Ishara ya msalaba  imekuwa ikitumika na Kanisa Katoliki, kama kisakramenti, hii ni maana ya tendo hilo!

1. Kukiri ukombozi wetu ulipatikana kwa Yesu Kristo kupitia msalaba

2. Kukiri utatu Mtakatifu yaani; Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu!

3. Tunaposhikanisha vidole vitatu wakati wa kufanya ishara ya msalaba, tunajiunganisha na Mungu katika nafsi tatu au tunapotumia vidole vyote vitano, tunakili madonda matano ya Yesu kristo!

4. Tunatumia mkono wa kulia kufanya ishara ya msalaba (unaomanisha mamlaka)

5. Tunapoanza kufanya ishara ya msalaba tunaanzia kwenye paji la uso kisha kifuani au kitovuni (ikimaanisha Mungu Baba alimtuma mwanaye kutoka juu mbinguni na kuja chini duniani)

6. Tunaelekea bega la mkono wa kushoto kisha kulia (hii inamaanisha yule aliyetumwa kutoka mbinguni kuja duniani, alitutoa katika uovu (kushoto) na kutuleta katika wokovu (kulia)

7. Baada ya kukiri vyote hivyo tunafunga mikono ambayo dole gumba hupishana kwa kutengeneza namna ya msalaba! Kama ishara kuu iliyotumika katika kumnyanyua yule tunaemwabudu yaani (Kristo Yesu)

Na mwisho tunasema "Amina" tukimaanisha iwe hivyo (yaani tudumu katika ukombozi huo).

Acha maoni yako hapo kisha share


No comments:

Post a Comment