WAKATI dirisha dogo la usajili linatarajia kufunguliwa Novemba 15, mwaka huu, beki wa zamani wa Yanga, Vincent Bossou, ameupigia magoti uongozi wa timu hiyo akiomba kurudishwa kundini hata bure.
Beki huyo ambaye hivi sasa anakipiga katika timu moja ya Mashariki ya Kati, ameomba kurejea Yanga kuwasaidia katika michuano ya kimataifa hapo mwakani.
Chanzo cha habari kutoka Yanga kilisema kuwa, Bossou ameomba kurejea kuichezea timu hiyo kipindi cha dirisha dogo baada ya mambo kumwendea ndivyo sivyo huko aliko kwa sasa.
“Ni kweli Bossou amekuwa na mawasiliano ya karibu na viongozi, ameomba kurudi tena Jangwani, sasa hilo ni suala la mabosi wa juu kuamua kumrudisha au kutokumrudisha,” alisema.
Tulimpotafuta Bossou kuzungumzia suala hilo, alikiri kuwapo na mipango ya kurejea tena kukipiga katika Ligi Kuu Tanzania Bara, huku akiipongeza Yanga kwa matokeo ya kutoka sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi Simba juzi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
“Nani kakwambia kuwa narejea kucheza tena huko? Ndio, nakuja Mungu akipenda na nimesikia juzi wametoka sare 1-1 Simba, si mbaya, ni matokeo mazuri,” alisema Bossou.
Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, alipoulizwa juu ya kurejea kwa beki huyo, alisema hana tatizo na kama suala hilo lipo, atalipeleka kwa Kamati ya Usajili ya timu hiyo kulijadili.
Hili suala ndio nalisikia kwako, ninavyojua mimi ni kwamba Bossou anacheza soka huko Mashariki ya Kati, ila kama anataka kurejea tena nitalifikisha suala lake mahali husika wafanye maamuzi,” alisema Lwandamina.
Bossou raia wa Togo alijiondoa kwenye kikosi cha Yanga katika kipindi cha dirisha kubwa la usajili mwaka huu, baada ya kugomea kusaini mkataba mpya kabla ya uongozi kumpa mkono wa kwaheri.
Katika safu ya ulinzi ya Yanga ya sasa, Kelvin Yondani na Andrew Vincent ‘Dante’, wameonekana kuelewana vilivyo hata pale mmoja wapo anapokosekana na nafasi yake kuchukuliwa na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Hivyo, iwapo Bossou atarejea Yanga, atakuwa ameongeza wigo wa uimara wa safu hiyo hasa kwa wakati huu timu hiyo inapopigania kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na ushiriki wao wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.
Wednesday, November 1, 2017
New
Aililia Yanga tena baada ya kuondoka msimu uliopita na je unakumbuka mchezaji huyu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment