Live:YANGA 2 vs WSC O UWANJA WA TAIFA>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Saturday, April 7, 2018

Live:YANGA 2 vs WSC O UWANJA WA TAIFA>>

MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAA
-Kuna mchezaji wa Yanga yuko chini baada ya kuumia
-Mahadhi anaingia na kuachia shuti kali kabisa
-Dawit anaachia mkwaju mkali kabisa, goal kick

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA

Dk 90 Ninja anamuangusha Jako kwenye kona ya 18 ya lango la Yanga, ni faulo
Dk 89 Dicha wanachonga kocha inaokolewa na kupata nyingine. Inachongwa tena, Elias anaruka na kupiga kichwa, goal kick
SUB Dk 88 Yanga wanamtoa Raphael Daud na nafasi yake anachukua Juma Mahadhi
Dk 88 Nafasi nyingine kwa Dicha, Yanga wako makini wanaokoa na kuwa kona
Dk 86 Martin yuko chini akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na beki wa Dicha


Dk 85 Dicha wanagongeana vizuri lakini mpira wa kichwa wa Dicha, Rostand anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 82, nusura Dicha wapate bao, lakini ni offside...Rostand yuko chini akipatiwa matibabu
Dk 81, Ajibu anaachia mkwaju wa chinichini, kipa anaokoa vizuri kwa mguu na kuwa kona, inachongwa na Dicha wanaokoa tena
Dk 80, Jako wa Dicha anaachia mkwaju nje ya 18 lakini ni nyanya kwa Rostand


Dk 79 Rostand anafanya kazi ya ziada mara nyingine kuokoa shuti na kuwa kona, inachongwa na Yanga wanaokoa vizuri kabisa
SUB Dk 76 Pato Ngonyani anaingia kuchukua nafasi ya Kamusoko ambaye ametoka pia
SUB Dk 74, Cannavaro anaingia kuchukua nafasi ya Dante aliyeumia
Dk 73, Rostand anapangua shuti kali ndani ya 18 na kuwa kuwa kona
Dk 70 Yanga wanagongeana vizuri lakini mwisho inakuwa hakuna faida

Dk 67 Buswita tena, nje ya 18 anajaribu lakini shuti nyanyaaaaa
Dk 67 Yanga wanaingia tena, Ajibu anachambua lakini pasi yake inaishia nyuma ya wachezaji wenzake


Dk 66 Yanga wanagongeana vizuri, Ajibu anapiga shuti kuuuuuuubwaaa
Dk 66 Kipa Dicha anafanya mbwembwe, nusura achome kibanda hapa
Dk 65, Mwinyi Haji anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira mbele ya Elias wa Dicha na kuwa kona, inachongwa tena inaokolewa
Dk 60, Mhilu yeye na nyavu, krosi safi ya Mwinyi lakini anapiga njeeee
Dk 55, Mhilu anaingia kwa kasi, Dicha wanaokoa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa


Dk 55, Mhilu anaingia kwa kasi, Dicha wanaokoa na kuwa kona, inachongwa na kuokolewa
GOOOOOOOOOO Dk 54, Martin anaruka na kufunga bao safi la kichwa pasi ya Mhilu
Dk 53 shuti kali la Elias, mara nyingine tena Rostanda anaokoa vizuri
Dk 52, mpira mrefu wa Martin, lakini Daud anachelewa na kipa wa Dicha anadaka kwa ulaiinii


Dk 47, Yanga wanaonekana kurejea nao wakianza kushambulia kwa kasi
Dk 45, Dicha wameanza kwa kasi wakishambulia kwa kasi wakionekana wamepania kupata bao la mapema


MAPUMZIKO


DAKIKA 2 ZA NYONGEZA


Dk 44, Daud anaingia vizuri anapiga krosi, inaokolewa na kuwa kona. Inachongwa na Ajibu, inaokolewa


Dk 42 Dicha wanagongeana vizuri tena ndani ya 18, lakini pasi ya mwisho iliyokuwa hatari, tayari Elias alishaotea
Dk 40 Jako anaachia mkwaju mkali ndani ya 18, Rostand anafanya kazi nzuri, anaokoa na kuwa kona
Dk 38, shambulizi jingine la Dicha kwa Yanga lakini Dawit anazuiliwa vizurrii na Ninja anaondosha safi kabisa
Dk 35 krosi maridadi ya Ajibu, Shaibu au Ninja anaruka na kupiga kichwa lakini ni goal kick


Dk 33, hakuna timu inaonyesha ina mipango imara zaidi ya bao, ingawa kila sehemu wanajitahidi kumiliki mpira zaidi
Dk 29, Kessy anaingia kwa kasi kubwa, hata hivyo krosi yake inakuwa haina macho, Dicha wanaokoa kupitia Alemayehu
Dk 28, Mhilu anaingia vizuri, Dicha wanatoa na kuwa kona, inachongwa inaokolewa
DK 24, mpira sasa unachezwa zaidi katikati ya uwanja na kila timu inaonekana kutokuwa na presha sana
Dk 20, Mhilu anaingia haraka kwenye lango la Dicha, anaachia mkwaju, kipa anadakana kutema, halafu anauchukua
Dk 18, Dicha wanacheza taratibu kwa kujiamini wakigonga pasi za mbwembwe na hili ni soka la kwao Ethiopia


Dk 20, Mhilu anaingia haraka kwenye lango la Dicha, anaachia mkwaju, kipa anadakana kutema, halafu anauchukua
Dk 18, Dicha wanacheza taratibu kwa kujiamini wakigonga pasi za mbwembwe na hili ni soka la kwao Ethiopia


Dk 16 kona maridadi ya Ajibu, beki anaokoa vizuri na kuwa kona tena, inachongwa na Ajibu, anapokea pasi ya Mwinyi, anaachia mkwaju wa chichini lakini goal kick
Dk 15 Martin anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, kipa anatema na beki anaokoa na kuwa kona
Dk 13, Dicha tena wanafanya shambulizi jingine lakini Yanga wanaokoa, ulikuwa mpira wa adhabu
Dk 9, Ajibu anaingia vizuri lakini analeta mbwembwe, anazuiwa vizuri kabisa
Dk 7, nafasi nzuri kabisa ya kupata bao, DAud na kipa, anapiga shuti kuuubwaaaaaa


Dk 5, Yanga wanapata kona baada ya kufanya shambulizi kali la kushitukiza
Dk 3, Dicha ndiyo wanaonekana kutawala mpira wakipiga pasi za chinichini na taratibu kabisa
GOOOOOOOOOO Dk 1, Yanga wanaandika bao kupitia Rapphael Daud, anaunganisha kwa kichwa krosi safi ya Ajibu
DK 1, Yanga wanaanza kwa kasi wakigonegeana haraka na inaonekana wamepania kupata bao la mapema

No comments:

Post a Comment