CHIRWA AREJEA NCHINI KWA MIKOGO TAYARI KWA KAZI HII>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Saturday, April 7, 2018

CHIRWA AREJEA NCHINI KWA MIKOGO TAYARI KWA KAZI HII>>


Straika wa Yanga, Obrey Chirwa tayari amerejea nchini tayari kuanza kuitumikia Yanga katika mechi za Ligi Kuu Bara, ikiwemo ile dhidi ya watani wao Simba, mwishoni mwa mwezi huu.

Chirwa alipewa ruhusa ya wiki moja kwenda kwao Zambia kutokana na matatizo ya kifamilia.

Lakini Chirwa amerejea nchini tayari kuendelea na kazi yake baada ya kuwa amemalizana na kilichomrudisha kwao Zambia.

Chirwa hatacheza mechi ya leo ya Yanga dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia ya kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwani ana kadi mbili za njano, hivyo kwa mujibu wa kanuni hatocheza.

Chirwa alipata kadi hizo katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers ya Boswana.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amethibitiwa kurejea kwa Chirwa ambaye ni tegemeo katika safu ya ushambulizi ya Yanga.

No comments:

Post a Comment