Baada ya kurejea nchini jana kikitokea Misri kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho, kikosi cha Simba kimepewa mapumziko ya siku nne.
Kikosi hicho kitapumzika kwa siku hizo 4 kuanzia leo mpaka Ijumaa, ambapo Jumamosi kitaanza tena mazoezi kujiandaa na michezo ya Ligi Kuu Bara.
Simba imerejea jana Dar es Salaam baada ya kushindwa kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho, kufuatia suluhu ya bila kufungana dhidi ya Al Masry SC.
Al Masry walifanikiwa kusonga mbele kutokana na faida ya bao la ugenini walilopata jijini Dar es Salaam ambapo mechi ilimalizika kwa sare ya 2-2.

No comments:
Post a Comment