SIMBA WAANZA HESABU KALI DHIDI YA NJOMBE MJI>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Friday, March 23, 2018

SIMBA WAANZA HESABU KALI DHIDI YA NJOMBE MJI>>

Kikosi cha Simba kinatarajia kuanza tena mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji FC kesho Jumamosi.

Simba watakuwa wanarejea kutoka mapumziko ya muda mfupi baada ya kutoka kushiriki mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kikosi hicho kilipewa mapumziko hayo Jumanne ya Machi 20 2018 baada ya kuwasili kikitokea Misri.

Simba iliondolewa na Al Masry kwenye Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kwenda suluhu ya mabao 0-0 ugenini huku wenyeji wakisonga mbele kufuatia faida ya bao la ugenini baada ya mchezo uliochezwa jijini Dar es Salaam kwenda sare ya mabao 2-2. 

Mazoezi hayo yatakuwa ni maalum kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Njombe Mji utakaopigwa Aprili 3 2018.

No comments:

Post a Comment