Baada ya Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, kunukuliwa akisema kuwa wamesitisha wamsitisha kuuza jarida lao ambalo walilianzisha likiwa ni maalum kwa kutoa habari za klabu hiyo, Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, ametamba kwa kusema kuwa zilikuwa ni mbwembwe tu.
Leo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara aliandika kuwa Yanga walianza kwa mbwembwe kuuza jarida hilo lakini hawajafika kokote, huku akiwakejeli kuwa wameuza kopi mbili pekee.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Afisa Habari wa Yanga, Dismas Teni, ameweka picha inayoonesha jarida la Yanga huku akiandika maneno ambayo inawezekana ikawa ni jibu kwa Manara.
"Maisha hayakosi changamoto! Unapomcheka mwenzio kwa sababu hajafanikiwa ni vyema ukaonyesha ulichonacho wewe" aliandika Ten.

No comments:
Post a Comment