MANULA NA ERASTO NYONI KUUNGANA NA WENZAO HUKO NJOMBE>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Wednesday, March 28, 2018

MANULA NA ERASTO NYONI KUUNGANA NA WENZAO HUKO NJOMBE>>

Wachezaji wa Simba waliokuwa wanaitumikia Taifa Stars wanatarajiwa kujiunga na kikosi cha Simba kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Njombe Mji.

Simba inajiandaa kucheza na Njombe Aprili 3 2018 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe, mchezo ambao ulikuwa ni wa kiporo.

Wachezaji hao waliokuwa Stars ni Erasto Nyoni, Aishi Manula, Shiza Kichuya, Shomari Kapombe pamoja na Said Ndemla.

Simba inaendelea na mazoezi jioni ya leo kwenye Uwanja wa Boko Veterani kabla haijakabiliana na Njombe Mji FC Aprili 3 2018.

No comments:

Post a Comment