HUYU HAPA KUTUA JANGWANI KUONGEZA NGUVU>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Thursday, March 29, 2018

HUYU HAPA KUTUA JANGWANI KUONGEZA NGUVU>>

Wakati Yanga ikiwa kwenye maandalizi ya kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United FC, taarifa za chini ya kapeti zinaeleza uongozi wa timu hiyo unataka kumsajili Mudathir Yahaya.

Yahaya anaichezea Singida United akitokea Azam FC kwa mkopo ambayo leo imetangaza kuwa mkataba wake umemalizika rasmi na yupo huru kwenda popote.

Kupitia kipindi cha michezo cha Radio One, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Yanga, Hussein Nyika, amesema wao kama klabu hawajazungumza na mchezaji huyo.

"Sisi hatujazungumza na Yahaya, akili yetu inafikiria mchezo ujao wa FA dhidi ya Singida United" alisema.

Aidha Nyika ameeleza kuwa yeye hana majukumu ya kusajili mchezaji bila Kocha kuamua kuamua, na endapo kama itatokea anahitajika, atatimiza majukumu yake.

No comments:

Post a Comment