Kiungo kinda wa Yanga Juma Mahadhi ameandika ujumbe mzito wenye dhamira ya kuwaomba radhi wapenzi wa soka hasa wanazi wap Yanga kwa kushindwa kwake kuwapa kile walichokitarajia toka kwake.
Mahadhi alisajiliwa kutoka Coastal Union ya Tanga ambako alionyesha uwezo mkubwa kabla hajatisha tena katika mechi za awali alipojiunga Yanga lakini baada ya muda alipotea na hakufanikiwa tena kurejesha kiwango chake.
Huu hapa ujumbe wenyewe
Assalam alykum ndugu zangu katika Imani haja yangu kwenu ni kuomba radhi kwa mashabiki wangu wote na wapenzi wote wa mpira wa miguu duniani, nakiri kufanya makosa hapo nyuma na nimejifunza mengi kupitia nyinyi nawaomba sana radhi.
Haja ya moyo wangu ni kutaka kufikia malengo yangu niliyojiweka lakini kwa mwaka 2017 ilikua ngumu sana kutokana na changamoto nilizokutana nao.
Sasa ombi langu kwenu Mashabiki, Viongozi na benchi la ufundi ni kwamba kijana wenu nahitaji msamaha kama niliwakosea bado nahitaji nafasi naamin siwezi kurudia kosa kwani nimejifunza mengi naahidi kuwa Mahadhi mpya naomba imani yenu kwangu na kama mnaona bado naitajika katika timu yangu pendwa Yanga SC.
Tumaini langu kilio changu kimewafikia nahitaji sasa kuanza mwaka mpya nikiwa kijana mwema na mpya.
Asanteni sana nawapenda wote.

No comments:
Post a Comment