ZANZIBAR HELLOS YAUNDIWA FIGISU CECAFA , HAWA WAPIMWA MKOJO NA KUCHULIWA HATUA - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Monday, December 11, 2017

ZANZIBAR HELLOS YAUNDIWA FIGISU CECAFA , HAWA WAPIMWA MKOJO NA KUCHULIWA HATUA




WACHEZAJI WA 4 WA ZANZIBAR HEROES WAPIMWA MKOJO, SASA WANASUBIRI MAJIBU KUTOKA AFRIKA YA KUSINI

Wachezaji wanne wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) leo saa 5 za usiku wamefanyiwa vipimo kama wanatumia dawa za kuongeza nguvu,vipimo ambavyo vimefanywa na Shirika la kupinga utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu Michezoni kupitia wakala wao wa nchini Kenya (World Anti-Doping Agency “WADA”) zoezi ambalo limefanyika katika Hoteli ya Garden waliyokaa kambi timu hiyo iliyopo Machakos Mjini Kenya.
Wachezaji waliyofanyiwa vipimo ni Kiungo Mohd Issa “Banka”, Fesal Salum “Fei Toto” na Washambuliaji Ibrahim Hamad Hilika na Suleiman Kassim


 Hofu hiyo ilopelekea kupimwa wachezaji hao imekuja kwenye Mashindano ya Cecafa Senior Chalenj Cup jioni ya leo katika uwanja wa Kenyatta Mjini Machakos mara baada ya kutoka sare ya 0-0 na Wenyeji Kenya na kupelekea Zanzibar kutinga moja kwa moja nusu fainali wakiwa na alama 7 wakiongoza kundi lao A lenye Mataifa kama Kenya, Libya, Rwanda na Tanzania bara.
WADA na CECAFA wameingiwa na wasi wasi kutokana na kiwango bora walichoonyesha Zanzibar katika Mashindano hayo huku ikiwaongoza mataifa kama Libya, Rwanda, wenyeji Kenya na Tanzania Bara ambapo WADA na CECAFA waliwafata wachezaji hao katika vyumba vya kubadilisha nguo baada ya kumaliza mchezo wa leo lakini hawakufanikiwa kuwapima jambo ambalo limepelekea kuwafata mpaka kambini kwao na kuwapima


Awali walisema Wachezaji wa Zanzibar wana mashaka nao na jinsi wanavyocheza si bure, hivyo baadae wakawataja wachezaji hao wanne akiwemo kiungo kinda Fesal Salum “Fei Toto” ambae leo amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo wa leo kati ya Zanzibar na wenyeji Kenya ulomalizika 0-0.
Vipimo hivyo vitapelekwa Afrika ya Kusini kisha majibu yatatoka badae.
“Tumeshawapima na hivi vipimo tunaenda navyo Afrika ya Kusini kisha tutaleta majibu baada ya miezi 6”. Alisema mmoja wa Afisa kutoka World Anti Doping.


 Kwa upande wa Zanzibar Heroes wameshangazwa na jambo hilo huku wakisema kuna mchezo mchafu unataka kufanywa na wenyeji wao.
“Sisi tuna wasi wasi na mchezo mchafu unataka kuchezwa hapa, Hoteli yao, chakula chao, maji yao na kutupima wanatupima watu wao, sawa sisi tumekubali kupimwa tunawasubiri na hayo majibu yao, mana hatuna wasi wasi wowote sisi”. Alisema Kiongozi mmoja wa Zanzibar.
Tangu kuanza Mashindano ya Cecafa ya mwaka huu Zanzibar inaongoza kutoa wachezaji bora wa mchezo yani Men of the Match ambapo mchezo wa awali Zanzibar Heroes waliichapa Rwanda mabao 3-1 huku mchezaji bora akitajwa kuwa Mohd Issa “Banka”, mchezo wa pili Zanzibar waliwafunga Tanzania bara mabao 2-1 na mchezaji bora wa mchezo akawa Ibrahim Hamad “Hilika” na leo Zanzibar 0-0 Kenya mchezaji bora pia katoka Zanzibar Fesal Salum.

No comments:

Post a Comment