YANGA KUTEST ILIOWASAJILI KESHO>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Saturday, December 16, 2017

YANGA KUTEST ILIOWASAJILI KESHO>>

Mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya Polisi Tanzania ambao awali ulipangwa kupigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, sasa utapigwa Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Akizungumza na waandihsi wa habari leo, Afisa wa Habari wa Yanga Dismas Ten amesema kuwa, mechi hiyo imesongezwa mbele kutokana na kuwa uwanja wa Taifanyasi zimepunguzwa sana nakuwa chini lakini pia Uwanja wa Uhuru Jumamosi unashughuli nyingine.

Tena amesema, pia wanaangalia endapo timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes ikifanikiwa kutinga hatua ya fainali kwenye michuano ya Cecafa nchini Kenya, huwenda Watanzania wengi watahitaji kuangalia mechi hiyo kupitia kwenye luninga, hivyo wanaweza kusogeza mbele muda wa mechi hata ikawa saa moja usiku.

"Tutatoa taarifa rasmi baadae baada ya kupata matokea ya Zanzibar Heroes na kujua kama wanacheza fainali au la, na hata hivyo mechi hiyo sasa itapigwa kwenye uwanja wa Uhuru Jumapili."

No comments:

Post a Comment