Saa kadhaa kabla ya kufungwa kwa dirisha dogo la usajili klabu ya Azam FC wamesema wamefunga pazia la usajili kwenye timu yao baada ya kumuongeza kikosini mshambuliaji wa kimataifa wa Ghana, Bernard Arthur kutoka klabu ya Liberty ya nchini Ghana.
Akizungumza na kipindi cha Mshikemshike Viwanjani cha Azam TWO, Afisa habari wa Azam FC, Jafari Idd Maganga amesema kikosi chao kimejitosheleza baada ya kumuongeza Arthur na hawana nafasi ya kumuongeza mchezaji mwingine.
Azam FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa baada ya kulingana pointi na Timu ya Simba na katika kujiandaa na ligi hiyo ambayo imesimama kwa muda, juzi ilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mvuvumwa United ya Kigoma katika dimba la Azam Complex na kuibuka na ushindi wa mabao 8-0.

No comments:
Post a Comment