MANJI TENA UYOO JANGWANI NA WANACHAMA WANENA , SIMBA WAJIVUNIA MO DEWJI - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Saturday, December 16, 2017

MANJI TENA UYOO JANGWANI NA WANACHAMA WANENA , SIMBA WAJIVUNIA MO DEWJI

Katika Mkutano wake na waandishi wa habari leo, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema Mfanyabiashara Yusuph Manji ambaye alijiuzulu nafasi yake ya uwenyekiti kutokana na matatizo yaliyomkumba,amerejea klabuni.

Mkwasa amedokeza kuwa Manji amesharejea klabuni na barua yake itajadiliwa kwenye Mkutano Mkuu utakaoitishwa ndani ya miezi mitatu.

"Mwenyekiti amesharejea klabuni na yupo nasi. Tusubiri mkutano Mkuu ili barua yake ijadiliwe na wanachama. Ndio wenye mamlaka ya kuamua hili kikatiba"

"Milango ipo wazi na kama atakuwa amepumzika na presha yake imeshuka basi klabu inamkaribisha kwa mikono miwili Tukutane kwenye Mkutano Mkuu ili tupate utamu zaidi," amedokeza Mkwasa.

No comments:

Post a Comment