WAZIRI wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dr Harrison Mwakyembe amebariki klabu zote za wanachama kuingia katika mfumo wa Hisa lakini amesisitiza kuwa sheria na kanuni ifuatwe kuwa ni lazima wawekezaji wamiliki Hisa asilimia 49 huku klabu ikibaki na asilimia 51.
Hivi karibuni Simba ilipitisha mfumo huo ambapo katika mchakato wao Mohamed Dewji ‘Mo’ alipita huku klabu ikibariki mwekezaji wao kuchukuwa asilimia 50 na klabu ikibaki na asilimia 50 ambayo ni makubaliano yao kama klabu.
Kauli hiyo ambayo ni kama inaurudisha nyuma mchakato wa uwekezaji huo Simba, ameitoa leo wakati wa makabidhiano ya vifaa vya michezo kwa klabu ya Stand United ambayo imepata udhamini wa Kampuni ya michezo ya kubahatisha ya Biko.
Leo Magazeti Ya
NA WA
Mh. Mwakyembe akishuhudia makabidhiano ya hundi kwa ajili ya udhamini wa Stand United
Mwakyembe alisema kuwa serikali haina tatizo na uwekezaji huo kwa klabu za wanachama lakini kila klabu inapaswa kufuata kanuni za Baraza la Michezo Nchini (BMT) ambazo zimefanyiwa marekebisho.
“Klabu zote za wanachama tunaziruhusu kuingia kwenye mfumo wa Hisa kikubwa tu wafuate kanuni za sasa ambazo zimefanyiwa marekebisho,” alisema Mwakyembe.
Taarifa hiyo inaweza kuwa hatua nyingine ya bilionea huyo wa Simba kurudi kutafakari upya kabla hajafanya maamuzi kama alivyofanya hapo awali ambao alihitaji 51% kabla ya klabu kukubali kumpa 50% ty ambazo nazo zimepigwa na serikali kwa mujibu wa kanuni.

No comments:
Post a Comment