LICHA ya Kamati ya nidhamu ya Klabu ya Yanga kumsamehe nyota wao wa Kimataifa Donald Ngoma kutokana na utovu wa nidhamu, inatarajia kumlima nusu ya mshahara wake wa mwezi mmoja.
Ngoma raia wa Zimbabwe amekuwa gumzo ndani ya vinywa vya mashabiki wa timu hiyo kutokana na kutokuwepo kwa muda dimbani na kuzua hofu miungoni mwao.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Klabu hiyo Hussein Nyika baada ya kusamehewa kwa kosa lake hilo na ili iwe fundisho kwa mchezaji mwingine amesema watamkata nusu mshahara wake wa mwezi mmoja.
“Ameomba msamaha hivyo sisi kama walezi tumeona tumsamehe tusonge mbele, licha ya msamaha huo atakatwa nusu ya mshahara wake wa mwezi mmoja, ili isijejirudia kwa wengine,” alisema Nyika.

Adhabu hiyo imemkumba Ngoma baada ya kuonyesha utovu wa nidhamu akiondoka kwenye timu bila kuaga na kukaa kwao zaidi ya mwezi mmoja licha ya viongozi kumtumia ujumbe ili arejee lakini alikuwa hajibu na alivyorejea alidai alienda kutibiwa kwa daktari wake na baada ya kumaliza akaanza kushughulikia hati ya kusafiria aliyodai kupotea.
Mbali na msamaha huo nyota huyo anatarajiwa kuwa nje ya dimba kwa wiki tatu hadi sita kutokana na ripoti ya daktari wake kufuatia kusumbuliwa na nyama za paja.
Hata hivyo toka Ligi kuanza Septemba mwaka huu nyota huyu amecheza mechi nne kati ya mechi 11 huku akiambulia kutikitisa nyavu mara moja pekee.

No comments:
Post a Comment