Mwisho wa usajili dirisha dogo ni leo saa 12:00 usiku hadi sasa vilabu vikubwa hapa nchini vimekuwa kimya na kile kinachoendekea kuelekea kufungwa kwa usajili huo, mashabiki wa timu hizo wanaitaji kufahamu nani anaondoka na yupi anaingia lakini cha kushangaza ni ushamba na ulimbukeni kwa viongozi wetu kwa kutowajulisha mashabiki wao kuhusu usajili wa timu zao pendwa, watanzania bado tupo nyuma kimaendelea wenzetu kwenye nchi zilizoendelea uwezi kukuta ujinga wa namna hii wa kutotangaza mchezaji unayemsajili au unayemuacha, hii inaleta picha mbaya na mashabiki kukosa imani na viongozi wao, ukweli na uwazi ni jambo moja muhimu sana mbele ya mashabiki ni vyema wapenzi na mashabiki wa timu husika kufahamu muenendo mzima wa timu yao pendwa lakini bado viongozi wa timu hizo wamekuwa awajitambui hata kidogo kwa kuwanyima haki za msingi mashabiki wao, leo usajili wa bongo umekuwa ni siri hivyo kupelekea mashabiki na wapenzi wa timu hizo kukosa furaha na amani moyoni, sidhani kama kuna tatizo kwa shabiki kufahamu usajili uliofanywa na klabu yake! Kwani hiyo ni haki yake ya msingi kulingana na mapenzi yake makubwa ndani ya klabu husika, sawa utasajili kwa siri lakini mwisho wa usajili wa siri ni mchezaji husika kuwa pumba yani mtupu hana chochote kipya matokeo yake ni viongozi kubeba lawama na matusi ya nguoni kutoka kwa mashabiki wa timu husika, sijui ni lini viongozi wetu watabadilika na kuweka kila kitu hadharani, kila siku ni muendelezo wa ujinga ule ule kwa viongozi wetu kutojitambua, mashabiki wa simba sc wanayo haki ya kufahamu nini kinaendelea ndani ya klabu yao hadi sasa kuelekea kufungwa kwa usajili wa dirisha dogo, wanaitaji kufahamu ni haina gani ya mchezaji aliyesajiliwa lakini bado viongozi wamekuwa kimya huku msemaji wa klabu akionekana kuongelea mambo mengine tofauti na mashabiki wanavyotarajia, ok sisi ni watoa tarifa kwa mashabiki lakini bado tunafanya makosa kwa sababu mwenye haki ya kutoa tarifa ni msemaji wa klabu lakini saa nyingine inatubidi tuingilie jukumu la msemaji kutokana na kuchelewa kutoka kwa tarifa ndani ya klabu hivyo kupelekea sisi kuchukua mamuzi ya kuwajulisha mashabiki wetu kwa kile kinachoendelea jambo ambalo sio sahihi, ila inapobidi tutaendelea kufanya hivyo ili kuondoa hofu na mashaka kwa mashabiki wetu, simba sc nguvu moja endelea kuwa nami..
Thursday, December 14, 2017
New
DILISHA LA USAJILI KUFUNGWA LEO , KLUBU HII INASAJILI TETESI TU>>
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment