LIPULI KWA ASANTE KWASI AKUBALI YAISHE , TSHISHIMBI WA YA ATOA NENO USAJILI BEKI MSIMBAZI>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Friday, December 22, 2017

LIPULI KWA ASANTE KWASI AKUBALI YAISHE , TSHISHIMBI WA YA ATOA NENO USAJILI BEKI MSIMBAZI>>




Tshishimbi atia neno kuhusu usajili wa Kwasi, aeleza anavyomfahamu

Kiungo wa klabu ya Yanga, Papy Tshishimbi ameibuka na kudadavua jinsi anavyomfahamu mchezaji aliye katika harakati za kutua katika Klabu ya Simba kwa sasa, Asante Kwasi ambaye aliwahi kucheza naye timu moja huko Swaziland na anachofahamu ni kwamba Mghana huyo hajawahi kuwa beki wa kati.

Tshishimbi amefunguka kwamba anachojua yeye kuhusu Kwasi kua ni beki wa pembeni pia ni winga mkali, hivyo anashangaa kusikia katua Msimbazi akiwa beki wa kati.ambapo amezidi kufunguka kwamba anamjua vyema mchezaji huyo kuliko mtu yeyote Tanzania na kilichomshtua ni kuona beki huyo akicheza nafasi ya beki wa kati kitu ambacho kimemshangaza.

Tshishimbi alisema Kwasi anayemjua yeye ni beki hatari wa kushoto na kwamba mbali na nafasi hiyo pia anajua kucheza vema winga ya kushoto na ukimpanga hapo anakuwa hatari kutokana na kujua kutupia kambani.

Alisema Kwasi aliwahi kutua Mbabane Swallows na kucheza naye kwa muda kabla ya kusepa zake, lakini hakuwa beki wa kati kama alivyomkuta Tanzania alipotua Jangwani katikati ya mwaka huu.

“Namjua vyema Kwasi, sidhani kama kuna mtu anamjua Kwasi kuliko mimi hapa Tanzania, niliwahi kucheza naye Mbambane lakini kuna mambo yalitokea akaondoka pale. Si beki mbaya sana,” alisema Tshishimbi.

“Unajua kilichonishangaza ni kuona Kwasi anacheza hapa Tanzania tena beki wa kati, tulipokuwa kule alikuwa anacheza beki wa kushoto na winga ya kushoto akicheza nafasi hizo anakuwa hatari sana.

“Akicheza winga tambua kwamba anaweza kufunga kutokana na kujua kutumia mguu wa kushoto, lakini sioni kama atatusumbua, hapa Yanga tuko sawa hata kama Simba itafanikiwa kumchukua.”

Tshishimbi alifichua kuwa wakati Yanga ilipotaka beki wa kati, alimuona Kwasi lakini aliamua kuwaletea Yanga beki mzuri zaidi Fiston Kayembe na kutamba mashabiki wa Yanga wajiandae kuona umahiri wa beki huyo mpya.

“Fiston ni beki imara kuliko Kwasi, hivyo kama nitakuwa nakuambia maneno ambayo hutaamini ngoja arudi na kuanza kazi hapa utakubali hiki ninachosema,” alisema Tshishimbi.

Simba inapambana kumvalisha Kwasi uzi mwekundu na mweupe baada ya kumnasa katika dirisha dogo, japo mabosi wa Lipuli wameshikilia bango kuwa mchezaji huyo ni mali yao na bado wana mipango naye.

Kwa sasa hatma ya Kwasi shakamilika na huko ndani ya Simba.

No comments:

Post a Comment