YANGA YAKUBALI YAISHE , KAMA UTANI VILE SASA AJIB KUNG'OKA NA HUYU HAPA JANGWAN>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Tuesday, November 21, 2017

YANGA YAKUBALI YAISHE , KAMA UTANI VILE SASA AJIB KUNG'OKA NA HUYU HAPA JANGWAN>>

KISHERIA iko hivi. Kama Yanga ikishindwa kulipa malimbikizo ya mishahara ya wachezaji wake ndani ya siku 10 zijazo, yeyote yule akiwamo Ibrahim Ajibu au Papy Kabamba Tshishimbi wana uwezo wa kuvunja mikataba yao na kusepa.


Habari za ndani zinasema kwamba wachezaji wa Yanga waliamua kujikaza kisabuni na kuficha hali hiyo ngumu wanayopitia katika siku za hivi karibuni na kuendelea kutupia tu kuweka kwanza mambo sawa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.


Lakini habari njema ambazo zimethibitishwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Boniface Mkwasa, ni kwamba kweli wachezaji wote wanadai mishahara, lakini alitoa kauli ya matumaini akisema wapo katika hatua za mwishoni na huenda leo Jumanne wakakamilisha kuwalipa malimbikizo hayo.


“Ni kweli wanadai, ila viongozi wanashughulikia jambo hilo, kesho (leo) Mungu akipenda wataanza kulipwa mishahara yao kwani tunatambua umuhimu wao katika timu,” alisema beki huyo wa zamani wa Jangwani hapo aliyewahi kuifundisha timu hiyo.


Habari zinasema kwamba hata ushindi wa mabao 5-0 walioupata juzi Jumapili dhidi ya Mbeya City, ulitokana na wachezaji na benchi la ufundi kutanguliza mbele maslahi ya timu, lakini ukweli wa mambo ndani yake kulikuwa na ukata mkubwa.


Mmoja wa wachezaji mahiri wa Yanga alidokeza kwamba hawaonja mishahara yao kwa zaidi ya miezi miwili sasa na kama juhudi za uongozi hazitafanyika ndani ya siku 10 zijazo, watatimiza miezi mitatu.


Alidai kwamba baadhi yao walianza kupiga hesabu za kuachana na timu hiyo kwa vile walikuwa hawaelewi nini kinaendelea, lakini kama mambo yakifanyika leo watu watacheka na shangwe litaendelea.


“Kwa upande wetu tumejitahidi sana kuvumilia,” alisema.


Sheria za Ajira zinasema kwamba endapo mwajiri atashindwa kuwalipa wafanyakazi wake kwa miezi mitatu mfululizo, hatua hiyo itakuwa ni sawa na kuvunja mikataba ambapo mwajiriwa anaweza kuondoka bila kizuizi chochote kujiunga na mwajiri mwingine.


Aliyekuwa Katibu Msaidizi wa Chama cha Wanasoka Tanzania (Sputanza), Abeid Kasabalala, alisema: “Klabu ambayo itashindwa kumlipa mchezaji wake katika miezi mitatu mfululizo, kisheria itakuwa imevunja mkataba wake. Ingawa pia inategemea na makubaliano yao kimkataba yakoje.”

Karibu

No comments:

Post a Comment