SIMBA YAWAVURUGA MASHABIKI WAKE, SASA WAMKINGIA KIFUA MO IBRAHIM>>>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Sunday, November 12, 2017

SIMBA YAWAVURUGA MASHABIKI WAKE, SASA WAMKINGIA KIFUA MO IBRAHIM>>>>

OMBI LANGU KWA SIMBA FANS...
hii timu bado haijauzwa. Ni mali ya wanachama
Na wanachama ni mashabiki namba moja wa Simba.
Hivyo basi tuna haki na wajibu wa kutoa maoni na kupaza sauti zetu hata zifike mahali sahihi.

Ndugu wana Simba mimi ni mmoja wa walioumia kwa kuondoka kwa Tambwe, na hivi karibuni nimeumia zaidi kuondoka Ajibu.
Niliumia sio kwakua hatuwez pata wengine.. Bali niliumia baada ya kuona wanaenda kwa mahasimu wetu... Na kiukweli Tambwe amewasaidia sana, kitu ambacho nakiona kwa Ajibu.
SIO VIZURI KUKUZA NA KUVILEA VIPAJI HALAFU UNAMPA ADUI UNAANZA KUPAMBANA NA VIFAA VYAKO MWENYEWE.
sasa hayo yamepita... Tugange yajayo.
Lakini kuhusu huyu dogo
Mo Ibrahimu....
Jamani tupige kelele zifike, huyu dogo apewe nafasi. Kama hawamtaki basi wampe nafasi wamuuze nje lakini asiende kwa watu ambao tunakimbizana kutafta ubingwa.
Kinachoniuma pia ni kua.... Wachezaji wakishaenda yanga... Wanazeekea hapo hapo. Ndoto za ulaya zinakufa. Wanawatumia mpaka damu ya mwisho. Simba tuamke.
#Omog #Play #Mo

No comments:

Post a Comment