KICHUYA WA SIMBA AMUOTESHA WIKI NZIMA ROSTAND WA YANGA, ASEMA KICHUYA NI ZAIDI YA WACHEZAJI WALOWAHI KUMFANYIA DHAHAMA ,FUATILIA YALIYOMKUTA BAADA YA KUTAMKA MANENO HAYO>>>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Saturday, November 4, 2017

KICHUYA WA SIMBA AMUOTESHA WIKI NZIMA ROSTAND WA YANGA, ASEMA KICHUYA NI ZAIDI YA WACHEZAJI WALOWAHI KUMFANYIA DHAHAMA ,FUATILIA YALIYOMKUTA BAADA YA KUTAMKA MANENO HAYO>>>>




*Rostand aweweseka kufungwa na Kichuya, aeleza siri ya bao lake*

LICHA ya siku tano kupita tangu lilipochezwa pambano la Watani wa jadi, mlinda mlango wa Yanga, Mcameroon, Youthe Rostand bado  anaonekana kuweweseka kutokana na bao alilofungwa staraika wa Simba , Shiza Kichuya, baada ya kueleza siri ya bao hilo. Rostand aliruhusu bao hilo lililofungwa na Kichuya dakika ya 57, ya mchezo huo baada shuti la Okwi na mpira kutua karibu na Erasto Nyoni aliyempenyezea pasi mfungaji, katika mchezo uliomalizika kwa sare bao 1-1 Jumamosi iliyopita. Kipa huyo zamani wa African Lyon amesema kuwa kabla ya kufungwa bao hilo aliwaambia mabeki wake wamlinde kwani upande aliokuwepo jua lilikuwa likimpiga usoni hivyo hakuwa akiuona vizuri mpira. “Upande niliyokuwa jua lilikuwa likipiga usoni hivyo haikuwa rahisi kuona mpira, shambulizi lile lilikuwa la kushtukiza japo nilipangua mpira,  lakini sikuwa nimeuona vizuri wakati unakuja ndo mana haukwenda  mbali , hata wakati kichuya anafunga sikuwa nimeuona mpira kutokana na  mwanga kuwa mkali, amesema Rostand.

By
*keira +2

No comments:

Post a Comment