HUYU NDIYE KOCHA TUPILIA MBALI OMONG, HUYU AIVUSHA YANGA KUTOKA KWENYE WIMBI HILI>>>> - KASULU WADAU BLOG

Breaking

ONLINE

Thursday, November 23, 2017

HUYU NDIYE KOCHA TUPILIA MBALI OMONG, HUYU AIVUSHA YANGA KUTOKA KWENYE WIMBI HILI>>>>

LWANDAMINA ANAVYO PAMBANA NA ROHO TATU.
Na


    …~First they ignore you,then they laugh at you, they fight you then you win.

Maisha ya mpira ni maisha ambayo yanahitaji subira, imani na uvumilivu wa hali ya juu.Hayo yote yatakuwa chini yanatafsiri nidhamu kama msingi mkuu wa maisha ya kila mwanadamu.Aliwahi kusema mtaalam mmoja ambae pia ni mwanafalsafa mkubwa sana,alisema kuwa katika harakati za kupambana kimaisha ili kupata mafanikio wale wanao kuangalia lazima watakuwa katika taswira tatu, "First they ignore you,then they laugh at you,then they figh you,then you win.

Mara nyingi huwa najifunza mengi kupitia kwa George Lwandamina (The chicken), kocha wa Young Africans.Ujio wake katika klabu hiyo ulitokana na kusitishwa kwa mkataba wa aliyekuwa kocha wa timu hiyo wakati huo,mholanzi Hans van de Pluijm.Lwandamina alifika Yanga katikati ya msimu wa league mwaka jana.Ameweza kupambana vilivyo mbali na matatizo aliyoyakuta lakini amefanikiwa kuiongoza Yanga kutetea ubingwa wake wa league ikikwa ni mara ya tatu mfululizo.

Msimu wa ligi uliisha na akafanya usajili wa kuwaongeza nyota kadhaa katika kikosi chake akiwa ameyafanyia kazi mapungufu aliyoyaona katika kikosi cha Yanga.

Amesajili golikipa (Rostand Youthe&Kabwili) na mabeki (Gardiel &Abdallah Shaibu) pia viungo (Pappy Tshishimbi,Daudi Raphael,Buswita Pius,Akilimali) na Ibrahim Ajib kule mbele katika eneo la final Third huku akiwa pandisha nyota Maka Erdward na Said Mussa toka kikosi cha vijana.

Huu ni usajili ambao umemsaidia vilivyo mzambia huyo hadi sasa akiwa na point 20 katika mechi kumi nyuma ya vinara Simba sc ambao wapo kibindoni na points 22 baada ya mechi kumi.

Mbali na matokeo hayo,mashabiki,wapenzi na wanachama wa mabingwa hao wamekuwa na wasiwasi dhidi ya mwalimu huyo tena wakionesha kutokuwa na imani nae kma baadhi ya mechi.Lakini Mwalimu huyo amekuwa mvumilivu na amejitahidi kuziba masikio yake huku akiamini kile anachokifanya.

Lakini ni vyema wengi wao wakatambua kua Ukocha ni taaluma kama taaluma zingine. Subira,imani na uvumilivu vinahitajika.Tena kuianda timu na kutengeneza mfumo ni process.It is not an overnight job, Lwandamina akalala na akiamka Young Africans ikacheza kama Mamelody sundowns au TP Mazembe.

George analaumiwa na kubezwa leo hii lakini bado amezidi kuonesha thamani yake kama mwalimu.Haya ni mambo ambayo Lwandamina anapambana nayo:-

1.IDADI YA MAJERUHI KATIKA KIKOSI CHAKE.

Moja ya mambo yanayo wakwamisha walimu kufikia kile walicho focus ni suala la injuries.Wachezaji wengi wa Young Africans hawana match fitness.Tena ni wale wachezaji muhimu wa kikosi cha kwanza (key-players.).Amekosa huduma ya professionals hawa Amis Tambwe,Donald Ngoma na Thaban Kamusoko.Wachezaji hawa wali deliver vitu muhimu sana katika kikosi cha Yanga msimu uliopita.Msimu umeanza Amis Tambwe hakucheza mechi hata moja, Donald na mwenzake Kamusoko walicheza mechi chache wakapata majeruha.Kama haitoshi katika mechi ya juzi amewakosa nyota wake muhimu kama kiungo Pappy Tshishimbi na Kevin Yondan lakini Pato na Nadir walitekeleza majukumu ipasavyo.
Sasa kwa hali hiyo Lwandamina angefanya nini? Lakini nimsifie mwalimu huyu kwani amekuwa mbunifu mno.Ameweza kuwaamini wachezaji waliopo na kuwapa nafasi ya kupambana vilivyo kupata matokeo.

2.HALI YA KIUCHUMI NDANI YA KLABU.

Ilifika kipindi fulani,timu ilipita katika wakati mgumu sana.Wachezaji waligoma kufanya mazoezi huku wakishinikiza uongozi wa timu hiyo kuwalipa maslahi yao.Ilikuwa ni wakati mgumu pia kwa mwalimu kutokana na programs zake kukwama.Masuala ya uchumi ndani ya timu yanachangia kwa asilimia kubwa either kuboresha or kuzorotesha performance ya wachezaji kwani ile morality huweza kuongezeka ama kupungua.

3.MAPUNGUFU MACHACHE KATIKA KIKOSI CHAKE.

Jambo lingine ambalo pia limegeuka mtihani mkubwa kwa Lwandamina,ni mapungufu ya baadhi ya nyota katika kikosi chake.

It's obvious kwamba baada ya kiungo Simon Msuva kutimkia kule Difaa Aljadida ya Morocco bado mwalimu huyo hajampata mtu ambaye ni expart na akaweza kudeliver kile alichokuwa akideliver Msuva msimu uliopita.Ni upande uliokuwa unazalisha magoli kwa asilimia kubwa.Lakini Lwandamina ameweza kuwa mbunifu mno kwa kumpa majukumu kiungo Pius Buswita kule pembeni japo hajaweza kufanya kile alicho kuwa akifanya Simon lakini matokeo yake amekuwa akicheza kama wing but sometimes akirudi kati kusaidia timu katika kupush mashambulizi.Japo hajaweza kupiga zile cross na kufanya overlapping kama Simon kipindi kile.

Vilevile kwenye safu ya ushambiliaji bado hajapatikana yule mtu atakae simama as a top striker na akafanya majukumu ya finishing hasa kwa zile pass nyoofu za Ibrahim Ajib.Mwalimu ameweza kumuamini Obbrey na kumpa majukumu japo asili yake sio mshambuliaji wa mwisho.Eneo lingine ni kwenye backline apatikane beki nne mwenye kujua majukumu na mkomavu haswa.Yanga wana mabeki wa mwisho wazuri mno na kama tulivyoona juzi baada ya kuumia Kevin,Nadir aliweza kuperform vizuri mno.

Sifa kubwa ya hawa mabeki wa mwisho ni positioning means ni muda gani anapaswa kuwa katika eneo sahihi tena kwa wakati na mwenye uwezo wa kuwaamrisha wenzake wakiwemo wale wa pembeni na yule msaidizi wake (sweeper).Akiwa na kasi ni kitu cha ziada kwake lakini kikubwa ni positioning.

Lwandamina akifanyia kazi hayo mapungufu machache hasa katika kipundi hiki cha dirisha dogo, hakika ataijenga Yanga ambayo wengi wanaipigia kelele.

Ni mwalimu mbunifu ambae alianza kuijenga timu kuanzia kwenye midfield,defensive line kuja kwenye forward line.

Mafanikio hayana shortcuts. Lazima conditions sahihi zifuatwe.Kutengeneza timu ni process.Na wakati huo:-

    …~First they ignore you,then they laugh at you, then they fight at you, then you win.

  ~....mwisho.

©Nisphory Buguja.

No comments:

Post a Comment